HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WAZIRI MWAKYEMBE AAPA KUTIKOMEZA MTANDAO TPA

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema kama kuna watu wanaopanga kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam ili kukwamisha mabadiliko yaliyoanza, watambue wanajisafishia njia ya kwenda kutumikia kifungo magerezani.
Dk Makyembe alisema mabadiliko katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), lazima yafanyike ili Bandari ya Dar es Salaam iweze kutoa huduma bora kuliko hata ile ya Mombasa nchini Kenya, hatimaye  kuleta tija katika pato la Taifa.
Alitoa onyo hilo jana alipokuwa akifungua mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi uliofanyika mjini hapa.
Alisema taarifa alizosoma kwenye baadhi ya magazeti jana, zikielezea mipango inayofanyika kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam kama ni kweli, basi waliopo katika mtandao huo wafahamu watanyofolewa mmoja baada ya mwingine na  kushughulikiwa kikamilifu, kwa sababu serikali sasa imechoka kuchezewa.
“Atanyofolewa kila mmoja anayejiona yupo katika mtandao wa kuihujumu Bandari ya Dar es Salaam, safari hii badala ya kuachishwa kazi watapelekwa jela,” alisema Dk Mwakyembe.
Waziri huyo alisema Bandari ya Dar es salaam inazungukwa na nchi sita jirani, ambazo zingetegemewa kushusha shehena zake hapo, lakini kwa sababu ya wizi uliokithiri na kuitia aibu nchi wanalazimika kuhamia bandari za mbali.
Alisisitiza kuwa atahakikisha anaisafisha Bandari ya Dar es Salaam ili iwe yenye kutoa huduma bora kuliko Mombasa, hatimaye kuleta tija na kuongeza pato la taifa.
“Bandari ya Dar es Salaam imegeuzwa shamba la bibi, watu wameunda mitandao ya wizi na ujanjaujanja ambao umeliletea aibu taifa letu, hatukubali tutahakikisha tunasafisha,” alisema.
Alisema kama taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari ni za kweli, basi mtandao huo uanze kusambaratika mara moja kwa sababu wahusika watambue wanashindana na serikali ambayo imejizatiti kukabiliana nao.
Kuhusu mkutano huo, Dk Mwakyembe aliwataka wafanyakazi walio chini ya wizara yake kufanya kazi kwa uzalendo na kuipenda nchi yao, watambue majukumu waliyonayo wamekabidhiwa na Watanzania ambao wanaitegemeakwa kiwango kikubwa.
Aliwapongeza watendaji wakuu wa Tazara TRL kwa kufanikisha usafirishaji wa abiria kwa treni mkoani Dar es Salaam, huku akisisitiza changamoto zilizojitokeza zitafanyiwa kazi.
Katibu mkuu wa wizara hiyo, Omari Chambo alisema changamoto iliyojitokeza baada ya kuanza kwa safari za treni Dar es Salaam, ni kujitokeza kwa abiria wengi ambao ni maradufu ya uwezo wa mabehewa yaliyotengwa.
Mwisho.

CHANZO:MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: