Imepita
muda sasa toka lilipotoka tangazo la kuwazuia watu wanaowatumia wanyama
kama usafiri wa kubebea mizigizo kuacha kufanya hivyo, lakini cha
kushangaza hadi sasa zoezi hilo halijafanyiwa kazi na wahusika kiasi cha
kuwafanya watu kuwatumia wanyama kama usafiri wao wa kawaida kama
anavyoonekana jamaa huyu pichani, (kushoto kwake) ni mwendesha Pikipiki
na kulia kwake ni mwendesha Baiskeli, wakiwa sambamba katika Barabara ya
Mwanakwerekwe, jana. Wengine utwakuta wakipakia mzigo mzito ambao hata
Pick up haiwezi kubeba lakini wao huwapakia wanyama hawa na kisha
kuwacharaza bakora ili waweze kutembea kwa mwendo kasi waweze kuwahi
kwenda na kurudia mzigo mwingine, jambo ambalo halifai kwa Haki za
binadam na wanyama pia.
Huyu naye katika Pikipiki Namba Z 893 DB akiwa kampakata mbuzi huku wakiwa katika mwendo.
Na je upakiaji wa mizigo na abiria kama hivi katika Chai Maharage hizi utakwisha zama gani?
Gari
la abiria likiwa limepakia abiria na mzigo mkubwa juu, huku likikatiza
mbele ya macha ya askari wa usalama barabarani bila kuonywa wala
kukamatwa, sasa hali hii itakwisha mjini Zanziba kweli?
PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO







No comments:
Post a Comment