JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA
LINAPENDA KUTOA WITO KWA WANANCHI WOTE KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA
KUUKARIBISHA MWAKA MPYA ITAKAYOADHIMISHWA USIKU WA TAREHE 3I/12/2012
KUAMKIA TAREHE 1/12/2013 KWA AMANI NA UTULIVU, PASIPO VITENDO AMA
VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI NA SHERIA ZA NCHI.
IKUMBUKWE KUWA, WANANCHI WENGI
HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUMSHUKURU MUNGU KATIKA NYUMBA ZA IBADA KWA
MAMBO MBALIMBALI AMBAYO MWENYEZI MUNGU AMEWATENDEA KWA KIPINDI CHOTE CHA
MWAKA.
PAMOJA NA HILO KUTAKUWA NA
MUENDELEZO WA SHEREHE HIZO KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA STAREHE. HATA
HIVYO, UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI YA WATU HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA
SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU.
JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA
HOFU WANANCHI WOTE KUWA, LIMEJIPANGA KIKAMILIFU. KUKABILIANA NA YEYOTE
YULE MWENYE NIA YA KUTENDA KITENDO CHOCHOTE CHA UVUNJIFU WA AMANI.
ULINZI UTAIMARISHWA KWENYE MAENEO YOTE YA IBADA, SEHEMU ZA STAREHE NA
MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.
AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA KWA
WALE WOTE AMBAO WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA HASA KWA MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO
KASI NA KUTUMIA VILEVI. TUTAKUWA WAKALI NA TUTAPIMA MADEREVA KILEVI.
KWA WALE WENYE KUMBI ZA STAREHE,
WAZINGATIE SHERIA NA UHALALI WA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI
WA WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI HIZO, BADALA YA KUENDEKEZA TAMAA YA
FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI.
VILEVILE, WAZAZI WAWE MAKINI NA
WATOTO WAO NA HASA DISKO TOTO AMBAZO ZIMEKATAZWA ILI KUEPUKA AJALI NA
MATUKIO MENGINE YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA JUU YAO. WASIRUHUSIWE
KUTEMBEA PEKE YAKE BILA KUWA NA MTU MZIMA.
JESHI LA POLISI LINATOA TAHADHARI KWA
WANANCHI WOTE KWAMBA, WATOKAPO KWENYE MAKAZI YAO WASIACHE NYUMBA WAZI
AMA BILA MTU NA WATOE TAARIFA KWA MAJIRANI ZAO, NA PALE WANAPOWATILIA
MASHAKA WATU WASIOWAFAHAMU WASIKAE KIMYA BALI WATOE TAARIFA KWA JESHI LA
POLISI ILI HATUA STAHIKI ZIWEZE KUCHUKULIWA HARAKA KWA WAHUSIKA.
MWISHO, WALE AMBAO HUPENDA KULIPUA
FATAKI (FIRE WORKS) WAHAKIKISHE WANATUMIA ZILE ZENYE MILIO MIDOGO KWANI
ZENYE MILIO MIKUBWA HULETA HOFU KWA TU HASA WAGONJWA AMBAO HUPATA
MATATIZO MAKUBWA ZAIDI. PIA NI MARUFUKU KUCHOMA MATAIRI BARABARANI,
KURUSHA MAWE KWENYE NYUMBA NA MAGARI YA WATU. SOTE TUTII SHERIA BILA
SHURUTI ATAKAYESHINDWA KUTOKANA NA SABABU ZAKE TUTAMSHURUTISHA KWA
KIWANGO KINACHOSTAHILI.
PICHA NA KAJUNASON BLOG



No comments:
Post a Comment