HUYU NDIYE PADRI ALIYEPIGWA RISASI USIKU WA SIKU KUU YA KRISMAS VISIWANI ZANZIBAR

 
Padri Ambrose Mkenda akiwa hospitalini.


Habari tulizozipata usiku wa  tarehe 25/12/2012  kupitia mtandao wa JamiiForums na Radio One, zinasema padri wa kanisa katoliki mjini Zanzibar Ambrose Mkenda amepigwa risasi na watu wasiofahamika akiwa anawasili nyumbani kwake ambapo watu hao wamepiga risasi akiwa getini ndani ya gari kuingia nyumbani kwake maeneo ya Kitomondo visiwani humo..

Ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo zinasema hali ya padri huyo si nzuri kwani risasi hiyo ilimpata maeneo ya mdomoni na kwamba kuna uwezekano wa kuhamishiwa bara kwa matibabu, huku watu waliofanya kitendo hicho wanadaiwa walikuwa wamepanda pikipiki wakiwa nje ya nyumba ya padri huyo wakisubiria afunguliwe geti kuingia nyumbani kwake. Hayo yanafanyika wakati ambao kanisa hilo duniani likiwa limetoa ujumbe wake mkuu wa Krisimasi usemao ''Upendo na Amani''.
 
Picha kwa hisani ya jamiiforum.com

No comments

Powered by Blogger.