Makaburi
UONGOZI wa Kanisa la Katoliki, Parokia ya
Kinyerezi Dar es Salaam unalazimika kugharimia ufukuaji wa makaburi
zaidi ya 15 ya Waislamu yaliyopo kwenye kiwanja namba 1370 kitalu B
kilichopo katika Kata ya Kinyerezi , baada ya kupewa kwa shughuli za
kijamii.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti
wa Parokia hiyo, Venance Kweka alisema wanalazimika kugharimia ufukuaji
wa makaburi hayo ili yaweze kuhamishwa kutoka katika kiwanja kupisha
shughuli nyingine za kijamii. Alisema tayari wamejiandaa kugharimia
shughuli hiyo kwa kuwa makaburi hayo ndiyo pekee yanayokwamisha kuanza
kwa mikakati ya ujenzi wa hospitali hiyo, ambayo kanisa linaamini
itakuwa ni msaada mkubwa kwa kinamama na watoto wanaoishi katika eneo
hilo la Kinyerezi.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa
Halmashauri ya Ilala Gabriel Fuime, ilifafanua kuwa itasimamia zoezi
hilo kwa Sheria ya Serikali za Mitaa( Mamlaka na Miji) ya mwaka 1982,
kanuni ya mwaka 2008 namba 4 c ambako itatumia wataalam wake.
Fuime katika taarifa yake hiyo alisisitiza ndugu na jamaa wa waliozikwa katika eneo hilo kuwasiliana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyerezi wakiwa na barua ya utambulisho kutoka kwenye ofisi ya Serikali ya mtaa wanaoishi kabla ya Januari 20 mwaka 2013.
Fuime katika taarifa yake hiyo alisisitiza ndugu na jamaa wa waliozikwa katika eneo hilo kuwasiliana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyerezi wakiwa na barua ya utambulisho kutoka kwenye ofisi ya Serikali ya mtaa wanaoishi kabla ya Januari 20 mwaka 2013.
Alibainisha kuwa makaburi hayo yanatarajiwa
kuhamishiwa kwenye makaburi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaliyopo
kata ya Kitunda eneo la Mwanagati Februari 9 mwaka 2013 baada
yataratibu zote kukamilika.
MWANANCHI
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment