Na: Albert Sanga, Iringa.
Leo
nitawapitisha wajasiriamali katika somo muhimu kuhusu rangi. Je,
unafahamu chimbuko la neno yeboyebo hapa nchini? Twende pamoja. Kampuni
moja ya nchini Tanzania miaka michache iliyopita imewahi kutambulisha
bidhaa zake za juisi zilizokuwa zikifahamika kama “Yebo” Juhudi kubwa
iliwekwa katika matangazo kutoa taarifa kwa watumiaji kuhusu uwepo wa
bidhaa hizo.
Juisi
ile ilikuwa ni ya rangi ya njano na katika matangazo ya kwenye
televisheni walikuwa wakitumika watu waliokuwa wamevaa kandambili za
plastiki zenye rangi ya njano. Kwa sababu kandambili hizo ndio kwanza
zilikuwa zinaingia sokoni zikabatizwa jina la yebo yebo.
Haikuishia hapo, neno ‘yebo yebo’ likawa linapewa kwa kila kitu chochote kilichoonekana kutumia ama kuwa na rangi ya njano. Timu ya mpira ya Yanga ilikuwa mmoja wa waathirika wa hali hiyo kwani ilibatizwa jina la Yebo yebo!

Yebo
yebo likajipatia urasmi wa ‘kiaina’ kutumika kwa ajili ya kumaanisha
kitu kinachopatikana kwa wingi, kisicho na thamani kubwa na
kinachodharaulika. Sina uhakika kampuni husika ilichukua hatua gani
baada ya hapo kujisalimisha na hatari ya bidhaa zao kuchukuliwa “poa”
kutokana na matangazo waliyoyabuni.
Ukifuatilia maarifa katika sayansi ya biashara utabaini kuwa tatizo la kuzuka kwa neno ‘yebo yebo’ halikuwa katika kandambili za plastiki wala halikuwa katika ubora wa bidhaa (kwa maana ya juisi yenyewe ukitoa ufungashaji) bali tatizo lilianzia katika rangi ya njano. Rangi ya njano ilipelekea kuzaliwa kwa dhana ya uyebo yebo kutokana na namna inavyotafsiriwa katika ubongo wa mtu.
Unapoona bidhaa yeyote ikiwa imefungashiwa kwa rangi za aina Fulani basi ujue jambo hilo halifanyiki kwa bahati mbaya bali linabeba maana kwa mtumiaji hata kama mtumiaji hajijui kwa nini anatumia bidhaa za rangi fulani na asitumie za rangi nyingine.
Ukiangalia
soda ya Seven Up kutoka kampuni ya Pepsi pamoja na soda ya Sprite
kutoka kampuni ya CocaCola utaona kuwa soda hizi zina rangi nyeupe
lakini zinafungashwa katika chupa za kijani, kwa nini?
Katika nchi nyingi masikini ikiwemo Tanzania, makampuni na wajasiriamali wengi wamekuwa hawatilii mkazo suala la rangi katika biashara zao. Hii inajumuisha katika bidhaa, mazingira ya huduma pamoja na rangi zitumikazo katika majengo ya kufanyia hizo biashara. Kupuuza suala la umuhimu wa rangi katika biashara kumepelekea wafanyabiashara na makampuni mengi kushindwa kukubalika miongoni mwa watumiaji.
Si kila rangi inafaa kupakwa katika kuta za duka, si kila rangi inafaa kutumika katika kuandika maandishi kwenye vifungashio vya bidhaa. Umakini wa kuzingatia athari za rangi miongoni mwa watumiaji kunatajwa kuwa ni moja ya sababu zinazosababisha bidhaa kutoka nje ya Tanzania kupendwa ukilinganishwa na za hapa nyumbani.
Kimsingi rangi zimethibitishwa kuwa na uwezo wa kushawishi saikolojia pamoja na tabia za watu. Mtaalamu mmoja wa saikolojia, Ward aliwahi kuulizwa njia za kuwezesha wafanyakazi kupunguza misongo wakiwa kazini. Alijibu, “Haihitaji semina wala mafunzo, jambo la msingi ni kupaka rangi sahihi katika kuta za vyumba wanamofanyia kazi, ambayo itaweka hamasiko ama mfifio kwa mabadiliko yanayohitajika”
Kwa mujibu wa mtafiti mwingine wa mambo ya biashara katika masoko, Wexner, anabainisha kuwa rangi nyekundu kwa mfano inatajwa kuwa inaambatana na hisia za kuhamasika, machungwa inaambatana na kukatishwa tamaa na kudharauliwa. Zambarau inaonesha hali ya kuthaminiwa, njano inawakilisha hali ya furaha, mzaha na kicheko na nyeusi inaonesha nguvu, umiliki na uimara.

Makampuni na biashara mbalimbali duniani kila siku zinakazana kutafuta njia za kuwezesha mwonekano na nguvu za nembo zao. Njia thabiti zinapovumbuliwa mikakati ya kimasoko huwekwa ambayo inahakikisha kuwa nembo hizo zinakuwa katika akili na fikra za wateja.
Tofauti
za kiutamaduni, kiuchumi, kijamii na nyinginezo zinaleta changamoto ya
ugumu kwa biashara na makampuni kufahamu kwa usahihi aina moja tu ya
nembo ambayo itawaridhisha na kuwapendezesha wateja wote. Hivyo biashara
nyingi hasa za kimataifa zinajikuta kuwa zinalazimika kuwa na nembo
moja katika muundo tofauti tofauti ili kufanikisha ufikaji wa bidhaa
kama ilivyokusudiwa.
Mbinu mojawapo ya kimasoko inayotumika na waendeshaji wa masoko hasa kimataifa bila kujali eneo ama watu gani wanaoenda kutumia bidhaa hizo ni rangi. Rangi ni moja ya vifaa ambavyo mameneja masoko hutumia katika kutengeneza, kuimarisha na kurekebisha mwonekano wa nembo katika ufahamu wa mteja. Umuhimu wa rangi kuwasilisha maana Fulani kwa walengwa kunathibitishwa hata katika taratibu na sheria mbalimbali duniani.
Kwa mfano kule nchini Marekani kuna sheria inayofahamika kama Lanham Act ambayo inalinda rangi za bidhaa kama nembo halali za kibiashara . Rangi zinafahamika kuwa zinabeba chembechembe za kihisia na kisaikolojia.
Maana
mbalimbali zinazoambatana na rangi mbalimbali zinaumaana mkubwa sana
kwa watu wanaohusika na masoko katika bidhaa ama huduma za makampuni
mbalimbali, kwa sababu mbinu za kutangaza bidhaa ndizo huamua
ukubalikaji wa bidhaa yenyewe.
Kwa mfano ua la waridi (rose) litabaki kuwa hivyo katika mataifa na tamaduni mbalimbali, lakini rangi za maua hayo zinakuwa na maana tofauti tofauti kutoka utamaduni, taifa moja kwenda jingine. Wajapan wanapendelea maua hayo yenye rangi nyeupe wakati watumiaji kutoka Hong Kong wanapendelea kutumia maua hayo ya rangi nyekundu
Mtu anapotaka kununua gari, rangi inatajwa na wataalamu wa masuala ya biashara kuwa inashika nafasi ya tatu katika orodha ya vigezo vya bei na ubora . Rangi pia ina umuhimu mkubwa sana katika ujenzi wa nembo ikiwemo logo, ufungaji na uonyeshaji .

Mtaalamu
na mtafiti wa mambo ya masoko, Wagner kupitia taasisi yake ya utafiti
wa mahusiano ya rangi na biashara, ijuliakanayo kama Wagner Color
Research Institute, alijaribu kuthibitisha dhana yake maarufu, ‘Colors
are associated with certain images’ (rangi inaambatana na taswira
fulani). Wagner alitumia kampuni inayoendesha migawaha iitwayo
Wienerschnitzel yenye matawi zaidi ya 350 katika nchi ya Marekani.
Wagner
aliishauri kampuni hii kuongeza rangi ya njano kidogo katika rangi
zinazopamba majengo ya migahawa yao ili kuwasilisha ujumbe kuwa kampuni
hiyo kupitia matawi yake inauza vyakula vya bei rahisi. Baada ya
kubadilisha rangi, kampuni hiyo iliripoti ongezeko la mauzo kwa asilimia
saba.
Kiujumla
rangi zinaambatana na taswira fulani kila inapoonekana na kufikiriwa
katika fikra za mteja. Kwa mfano rangi ya bluu mahali pengi huambatana
na maana na taswira ya utajiri, uaminifu na usalama. Ndio maana
ukifuatilia kwa umakini utagundua kuwa benki nyingi zinapenda kutumia
ama kujumuisha rangi ya bluu katika nembo na machapisho yao.
Hii
inaingiza taswira miongoni mwa wateja wa mabenki hayo kuwa, benki ipo
imara (utajiri mkubwa), ina umaninifu, (hivyo akaunti zake haziwezi
kufanyiwa hujuma), na usalama, (kimbilio sahihi la kutunzia hazina
zake). Wakati rangi ya njano inabeba mwonekano wa kitu cha bei rahisi
Wasimamizi wa masuala ya masoko katika makampuni na biashara wanapaswa kufahamu maana tofauti tofauti zinazoambatana na rangi ambapo maana hizo zitawezesha kugawanya na kupoka fursa mbalimbali za kimasoko kwenye jamii na tamaduni mbalimbali. Muunganiko wa rangi katika kufungasha bidhaa nao una umuhimu mkubwa sana ili kuwateka wateja.
Upo mfano mwingine wa kampuni ya kutengeneza vifaa vya kompyuta ya Apple kupitia bidhaa zake za iMac inafungasha kutumia mwunganiko wa rangi tano ambazo zina maana tofauti tofauti katika mataifa mbalimbali. Rangi hizo ni kijani, dhahabu, nyeupe, bluu na njano. Bidhaa za iMac zinapoingia Taiwan zinatafsiriwa kuwa ni amani, rafiki (kijani), zisizo na madhara (bluu na nyeupe), endelevu (dhahabu), zinazosisimua, zinazofanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi (njano).

Muunganiko
huo wa rangi unapoingia China tafsiri inakuwa ni nyingine kabisa lakini
bado tafsiri inaisaidia na kuiwezesha kampuni kuuza bidhaa zake vizuri.
Kule china bidhaa za iMac huleta maana ya; amani (kijani), nzuri na
zinazoleta urembo (njano) wakati nyeupe huwakilisha vitu vilivyo katika
mpangilio na vinavyofafanulika.
Kuna changamoto kubwa inayowakabili wajasiriamali wa Tanzania hasa katika wakati huu ambao tupo katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Namna bidhaa zetu zinavyotengenezwa na kufungashwa zinaamua sana jinsi zinavyoweza kushindana katika masoko ya kimataifa.

Hata
wafanyabiashara wadogo wadogo katika maduka na vibanda vyao ni vema
sana wakawa na ufahamu wa namna ya kupaka rangi zitakazowavutia wateja
na kuongeza uhakika wa kushinda changamoto za kiushindani!

No comments:
Post a Comment