Kikundi cha Jumuiya ya wanafunzi nchini India wakiwa wameshika mabango
wakati wa maandamano ya kupinga vitendo vya ukatili likiwamo kitendo cha
ubakaji kilichofanywa kwa mwanamke aliyefariki. Picha na AFP
NEW DELHI, India
MWILI wa mwanamke wa India ambaye amefariki
hospitalini nchini Singapore baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi
umerejeshwa nchini humo kwa ndege maalumu ya kukodi.
Balozi wa India nchini Singapore, T.C.A
Raghavan aliwaambia waandishi wa habari jana, saa kadhaa baada ya
mwanamke huyo kufariki kutokana na viungo vyake kushindwa kufanya
kazi katika hospitali nchini Singapore ambako alikuwa akipatiwa
matibabu.
Mwanamke huyo na ndugu wa marehemu walisafirishwa
kwenda India katika ndege maalumu ya kukodi mchana wa jana Jumamosi,
kwa mujibu wa Raghavan.
Waziri Mkuu wa India, Manmohan Singh alisema
kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mwanamke huyo ambaye alifanyiwa
vitendo vya kinyama kwa kubakwa na kundi la vijana na kwamba
maandamano yaliyozuka kutokana na kitendo hicho “yanaeleweka”.
“Nimesikitishwa mno kufahamu kuwa mwathirika
huyo wa mashambulizi ya kinyama yaliyofanyika Desemba 16 mjini New
Delhi ameshindwa kunusurika kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata
baada ya shambulio dhidi yake, “ aliandika waziri huyo mkuu katika
tovuti yake.
“Tumeshaona hisia na nguvu ambazo tukio hili
limesababisha. Hii ni hali ambayo inaeleweka kutoka kwa vijana wa
India ambao wanataka mabadiliko ya kweli.
“Nataka kuwaambia, familia yake na taifa kwa jumla kuwa amepoteza maisha, ni juu yetu wote kuhakikisha kuwa kifo chake hakitakuwa cha bure.”
“Nataka kuwaambia, familia yake na taifa kwa jumla kuwa amepoteza maisha, ni juu yetu wote kuhakikisha kuwa kifo chake hakitakuwa cha bure.”
India imetikiswa na maandamano makubwa tangu
msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 aliposhambuliwa kinyama katika
basi mjini New Delhi na kundi la watu sita.
Serikali imekuwa ikijaribu kulituliza wimbi la
hasira kwa kuahidi adhabu kali kwa uhalifu mkubwa unaohusiana na ngono
pamoja na kuunda tume maalumu ya uchunguzi kuhusiana na jinsi ya
kushughulikia kesi za ubakaji.
Wakati maofisa wakijitayarisha kwa ghasia zaidi
mitaani, polisi waliongezwa katika eneo la kati la mji mkuu wa India
kabla ya mwili wa msichana huyo kurejeshwa nchini humo jana.
Ofisa wa polisi wa mjini New Delhi, alihimiza watu
kuomboleza kifo cha mwanamke huyo kwa amani wakati maeneo kadha
ya mji huo mkuu yamefungwa.
Singh, ambaye hapo kabla alitoa wito wa
utulivu , alisema kuwa itakuwa, “Heshima kubwa kwa kumbukumbu yake
iwapo tutaweza kuelekeza hisia zetu hizi na nguvu katika kuchukua
hatua sahihi. Kwa muda huu tunahitaji mjadala wa maana na uchunguzi
kuhusiana na mabadiliko ya lazima na haraka ambayo yanahitajika katika
mtazamo wa jamii.
“Ni matumaini yangu kuwa tabaka lote la kisiasa pamoja na jamii yote itatenga maslahi yao finyu ya binafsi na ajenda ili kutusaidia kufikia hatima ambayo tunaikusudia, na kuifanya India kuwa mahali bora na salama kwa wanawake kuweza kuishi.
MWANANCHI
“Ni matumaini yangu kuwa tabaka lote la kisiasa pamoja na jamii yote itatenga maslahi yao finyu ya binafsi na ajenda ili kutusaidia kufikia hatima ambayo tunaikusudia, na kuifanya India kuwa mahali bora na salama kwa wanawake kuweza kuishi.



No comments:
Post a Comment