Msanii
wa kike anaechipukia na kung”ara katika fani ya muziki nchini
Tanzania, Mwanaisha Nyange (a.k.a- Dyana) akiongea na waandishi wa
habari (hawapo) pichani Dec, 28,2012 jijini Dar es Salaam ,
ametoa shukranii zake kwa Aljazerra Entertaiment kwa kumsaidia kumtoa
msanii huyo kimuziki , bila ya kuwasahau, wadau mbalimbali wote wa
muziki nchini ambao amesema ndio waliomsaidia kumfikisha hapo alipo
sasa katika sanaa hii ya muziki huu wa kizazi kipya , kwani bila ya
kupata ushirikiano wao asingeweza kufikia hapa alipo. . (kushoto) ni
Msemaji wa Aljazerra Entertaiment Simon John
Msanii
Richie Mavoko (a.k.a) kulia, pamoja na Msanii Mwanaisha Nyange
(kushoto) a.k.a- DYANA wakionyesha minjonjo mbele ya waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wakitoa shukrani kwa
wadau wa muziki nchini kwaniaba ya kampuni ya Aljazerra Entertaiment
ambayo ilianza kazi zake 01-04-2004 za kuwa saidia wasanii mbalimbali
wenye vipaji vya kuimba, kucheza na maagizo. Hadi sasa imefanikiwa
kumtoa kisanii (kujulikana na mafanikio) Diamond Plutim, Sam wa Ukweli,
Dyana, na Richie Mavoko na wengine wengi,(Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Msanii
Richard Lusinga (a.k.a – Richie Mavoko) akiongea na waandishi wa
habari hawapo pichani Dec,28,2012 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa
shukrani kwa niaba ya Kampuni yake ya Aljazerra Entertaiment, katika
shukurani zake amesema,” kama msanii wa kizazi kipya amewomba radhi
kwa wote aliowakosea na yeye pia amewasemehe” Pamoja na Kushukuru
kampuni ya Aljazerra Entertaiment, waandishi wa habari na wadau wote wa
muziki nchini, kwani ndio waliomfikisha hapo alipofikia na kuahihidi
atazidi kuboresha na kuwaletea nyimbo kali zaidi washabiki wake katika
mwaka wa 2013.Richie Mavoko anatamba na nyimbo zake kama Mbona
silai,Folo folo me,one time na Mery me . (kushoto ) Ni Msanii Mwanaisha
Nyange (a.k.a DYANA)



No comments:
Post a Comment