HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WASANII WA BONGO FLAVOUR WENGI HAWAKUTOKEA KWENYE MAZISHI YA MAREHEMU SHARO MILIONEA

Marehemu Hussein Ramadhani ‘Sharo Milionea’ (27)  
 
Ikiwa zimepita siku chache tangu tasnia ya burudani tanzania kuingia katika majonzi baada ya kumpoteza mchekeshaji na mwanamuziki Hussein Ramadhani Mkieti maarufu kama Sharo millionea tetesi zilizopo ni kwamba wasanii wa bongo flavour hawakuonesha sapoti ya kutosha katika msiba wa marehemu Shaomillionea.

Inasemekana kuwa wasanii wengi wa muziki huu BONGO FLAVOUR hawakujitokeza katika msiba wa marehemu kitu ambacho kimeleta maswali mengi kwa wananchi wakati enzi za uhai wake marehemu alikuwa mstari wa mbele kutoa misaada kwa wasanii wenzake kwa mara nyingi amekuwa akionekana maranyingi katika video zao hivyo
kufanya video hizo kupendwa kutokana na ubunifu aliokuwa akiuonesha.

Baadhi ya wasanii ambao tuhuma za kutohudhuria msiba ni Dully,Diamond,Ommy Dimpoz, Lady Jaydee, Barnaba, Liner, Dyner na wengineo wengi.Lakini kwa hawa niliowataja wametaja sababu zilizopelekea kutohudhuria msiba huo.

Katika show ya Friday Night Live FNL inayorushwa na EATV kila siku ya ijumaa wakijibu swali waliloulizwa kwanini hawakuhudhuria msiba kila mmoja alikuwa na haya ya kusema:

DULLY
''Mimi kwanza ulipotokea ule msiba na mimi nilikuwa nimefiwa na pia mimi nina presha mbaya sana so! nikaogopa sana kwenda huko''.

DIAMOND
''Yaaa! wakati msiba wa sharo millionea unatokea mimi nilikuwa safarini nikielekea kenya lakini nilimtuma blogger wangu na kumlipia nauli na gharama zote akiwa kule''.


OMMY DIMPOZ
''Siku ile ambayo sharo alikuwa anazikwa nilikuwa na appointment ya kufanya interview na ubalozi sasa si unajua ubalozi tena kuhairisha appointment ni siku mbili kabla so! ndio maana nikashindwa kuhudhuria''.

Kiukweli tabia iliyooneshwa na wasanii wa bongo flavour si nzuri kwasababu ukilinganisha na wasanii wa bongo movie coz bongo movie walivyoonesha ushirikiano katika msiba wa sharomillionea ni kitu kizuri,bongo movie walikuwa kwenye msiba wa John s Maganga lakini siku ileile walifunga safari hadi tanga kumzika mwenzao marehemu sharomillionea.
                                 
   ''KWELI UKIFA DHAMANI YAKO INASHUKA'' 
 
CHANZO: MAU2NDU BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: