Wamama wakiwa na watoto wao baada ya kujifungua.
ZAIDI ya watoto 140 wamezaliwa katika mkesha wa
kuamkia Sikukuu ya Krismasi katika hospitali za wilaya tatu ikiwamo
hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa watoto hao ni kutoka katika hospitali
ya Temeke ambayo idadi yao ni 53 ambapo wasichana ni 24 wavulana 29 na
kati yao pacha ni mmoja.
Kutoka katika hospitali ya Amana wavulana ni 32 na
wasichana 30 ni na mmoja wao ni pacha katika hospitali ya Taifa watoto
watatu ambao kati yao wawili ni wavulana na msichana mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Daktari wa zamu
katika hospitali ya Amana, Pendo Kataponda alisema ni kawaida kupokea
wajawazito na kuwahudumia kipindi cha Krismasi kama ilivyo kwa siku za
kawaida.
Kutoka hospitali ya Mwanayamala idadi ya watoto
waliozaliwa kwenye mkesha huo ni 25 ambapo kati yao wasichana ni 10 na
wavulana ni 15.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi waliojifungua
katika mkesha huo walielezea furaha zao ambapo walisema wanamshukuru
Mungu kwa kuwatunuku zawadi hizo.
Walisema kuwa hali zao na afya zao watoto wao ni
za kuridhisha kitendo ambacho kiliwafanya washindwe kuficha hisia zao za
furaha waliyo kuwa nayo.
Mbali na kushukuru walitumia fursa hiyo kupaza
sauti zao kuwataka wanawake wenye tabia za kutupa watoto kuacha mara
moja kwani wanamuasi Mungu.
Mwasiti Omary mzazi kutoka katika Hospitali ya Temeke alisema kumekuwa na habari nyingi kuhusiana na kutelekezwa kwa watoto ama kutupwa kabisa ni jambo la kulaaniwa.
Mwasiti Omary mzazi kutoka katika Hospitali ya Temeke alisema kumekuwa na habari nyingi kuhusiana na kutelekezwa kwa watoto ama kutupwa kabisa ni jambo la kulaaniwa.
“Ni bora kama hutaki kuzaa ukatumia kinga au
ukaacha kabisa kushiriki tendo la ndoa kuliko kuwatupa watu wasiokuwa na
hatia “aliongeza.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment