Askofu
Msaidi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa (katikati)
akiongoza ibada ya mkesha wa Sikuu ya Krismasi katika Kanisa la
Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Paroko
wa kanisa hilo, Padri, Joseph Mosha.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex
Malasusa akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Krismasi leo.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex
Malasusa akitoa baraka kwa waumini wa Usharika wa Azania Front baada ya
ibada ya Krismasi
Mmiliki
wa Mtandao wa Kijamii wa Kimbunga Net, Dotto Mwaibale akipeana mkono
na Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Alex Malasusa baada ya ibada ya Krismasi
iliyofanyika leo katika Usharika wa Azania Front.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex
Malasusa akiwa amembeba mtoto, Prisca John Mkony, Kushoto ni Sia
Robinson na Jane Mkony akiwa amembeba mtoto, Patricia.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph wakiwa katika ibada ya Sikukuu ya Krismas.
Mkurugenzi wa Free Media Ltd, Liliani Mtei (kulia) akiwa na baadhi
ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu wa kanisa hilo, Dk
Alex Malasusa (hayupo pichani) wakati wa ibada ya Krismasi
iliyofanyika.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex
Malasusa akipeana mkono na muumini wa kanisa hilo, Sevestine Mtunga
baada ya ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika kanisa la
Azania Front jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya akinamama waliojifungua wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismasi
wakiwa na watoto wao katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es
Salaam jana. Kutoka kushoto ni Fatuma Shaban mkazi wa Vingunguti, Lucy Dominick mkazi wa Mwananyamala na Moshi Mengi mkazi wa Manzese
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex
Malasusa akitoa Baraka kwa mtoto, Patricia John Mkony mara baada ya
ibada ya Sikukuu ya Krisimasi iliyofanyika katika kanisa la Azania Front
jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Rubani Mkuu mstaafu wa Serikali, Kapteni John Mkony, Jane John na Sia Robinson.
Sehemu
ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia mpya ya Mt. Bonaventure,
Kinyerezi wakifuatilia sehemu ya ibada ya Krisamsi iliyokuwa ikiendeshwa
na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp
Kadinali Pengo, Dar es Salaam leo.
Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo
akipokea michango mbalimbali ya fedha kutoka kwa viongozi wa jumuiya za
kikristo katika jimbo la segerea, dar es salaam alipokwenda kuongoza
ibada ya Krismasi sambamba na uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt.
Bonaventure, Kinyerezi, Dar es Salaam leo.
PICHA NA HABARI MSETO BLOG
No comments:
Post a Comment