Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijiandaa kukabidhi
msaada wa Vitanda 38 pamoja na Magodoro na Mashuka yake kwa Hoapitali
Kuu ya Mnazi Mmoja.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwajulia hali watoto
waliolazwa kupatiwa huduma katika wodi ya ajali Mnazi Mmoja kabla ya
kukabidhi msaada kwa ajili ya wodi hiyo.
Balozi
Seif akimkabidhi Muuguzi Mkunga wa Wodi ya Watoto waliopata ajali Bibi
Leluu Omar Said msaada wa vitanda 14, magodoro na mashuka kwa ajili ya
wodi hiyo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifuatana na Waziri wa Afya
Mh. Juma Duni Haji, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Saleh Mohd Jidawi na
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika Mh. Haroun
Ali Suleiman wakiangalia msaada wa vitanda, magodoro na mashuka
yaliyotolewa na msamaria mwema katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpa pole mmoja wa wagonjwa
wa wodi ya Mifupa aliyelazwa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa
vilivyotolewa na wasamaria wema.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi Muuguzi dhama wa
wodi ya Mifupa Bibi Afsa Abdulla msaada wa vitanda 24, magodoro na
mashuka kwa ajili ya wodi hiyo.
Wafadhili
na washirika wa Maendeleo wameendelea kukumbushwa kuchangia huduma za
afya kwa nia ya kuwaondoshea mzigo wananachi pamoja na Serikali katika
upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Kumbusho
hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi, wakati akikabidhi Msaada wa Vitanda 28 pamoja na Magodoro, Mito
na mashuka kwa ajili ya Wagonjwa wanaolazwa katika Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja.
Msaada
huo wa Vitanda unaokadiriwa kugharimu shilingi za Kitanzania Milioni
12,000,000/- unazihusu wodi ya Watoto wanaopata ajali, Wodi ya Mifupa ya
wagonjwa wa Kiume pamoja na chumba wanacholazwa wagonjwa wanaotumikia
chuo cha mafunzo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Akikabidhi
msaada huo uliotolewa na Wasamaria wema, Balozi Seif amesema bado
Hospitali pamoja na Vituo vya afya hapa Nchini vinahitaji kupatiwa
misaada ili viweze kutoa huduma katika kiwango kinachokubalika.
Amesema
Serikali kwa upande wake itaendelea kujitahidi zaidi katika kutafuta
wafadhili sambamba na kuongeza nguvu za upatikanaji wa vifaa vya huduma,
lengo likiwa ni kuimarisha huduma za afya mijini na Vijijini.
Msaada
huo unafuatia ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyoifanya
katika sekta ya afya mwaka uliopita na kushuhudia changamoto kadhaa
zinazovikabili vituo vingi vya afya, pamoja na Hospitali ukiwemo uhaba
na uchakavu wa vitanda na magodoro ya wagonjwa.
Wakipokea
msaada huo kwa nyakati tofauti Muuguzi Mkunga katika wodi ya Watoto
Bibi Leluu Omar Said na Muuguzi dhamana katika Wodi ya Mifupa ya
Wagonjwa wa Kiume Bibi Afsa Abdulla, wamewashukuru wafadhili hao kupitia
Balozi Seif kwa msaada wao utakaosaidia kupunguza matatizo
yanayozikabili hospitali hiyo.
Wauguzi
hao wakuu wa wodi hizo wameahidi kwa pamoja kuvitunza Vifaa hivyo ili
vidumu kwa muda mrefu kwa vile changamoto hiyo lilikuwa kilio chao cha
muda mrefu.
Hata
hivyo wauguzi hao wameiomba serikali kufanya utaratibu wa hifadhi zaidi
ya magodoro hayo ili yadumu zaidi suala ambalo Balozi Seif ameuagiza
Uongozi wa Wizara ya Afya kulifanyia kazi mara moja.
Mapema
Balozi Seif alipata fursa ya kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika
wodi zilizofanikiwa kupata msaada wa Vitanda, magodoro pamoja na
Mashuka.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anatarajiwa kutoa
msaada kama huo hivi karibuni katika Hospitali za Micheweni na Vitongoji
Kisiwani Pemba.
PICHA NA MO BLOG



No comments:
Post a Comment