Wananchi wakimgombania kibaka huyo kama mpira wa kona.
Mwananchi huyu mwenye hasira kali akimnyanyua juu kibaka huyo na kumtupa chini kama akina 'John Cena'.
Kichapo kikiendelea kwa kibaka huyo.
Kibaka huyo akizidi kuhukumiwa mtaani.
Ustadhi akijaribu kumnusuru kibaka huyo.
Ustadhi huyo aliamua kuondoka na kibaka ili kumwokoa.
Wananchi walikuwa bado wanampa kichapo wakati akipelekwa kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani.
..............................................
KIJANA mmoja anayesadikiwa kuwa ni kibaka mchana wa jana alinusurika kifo
baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananachi wenye hasira
wakimshutumu kuiba watoto wadogo na kwenda nao eneo la mto Morogoro
chini ya daraja la Shani na kuwafanyia vitendo vya kihuni.
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa
jina la Juma Athuman alidai kwamba kijana huyo ana kawaida ya kuwateka
watoto wadogo hasa wa shule na kuwapeleka chini ya daraja hilo na
kuwafanyia vitendo vya kihuni.
" Kwa kipindi kirefu tulikuwa tukimsaka kibaka huyu ambaye ana tabia ya
kuwateka watoto wadogo na kuwapeleka mto wa Morogoro chini ya daraja la
Shani.
"Muda huu tumemfuma akiwa chini ya daraja hilo na mtoto mdogo ndipo
tulipomfukuza na kufanikiwa kumkamata eneo hili la kituo cha mafuta
jirani na daraja hili la Shani," alisema Juma Athuman.
Katika hatua nyingine 'ustadhi' mmoja alijitosa na kumnyakua kibaka huyo
kutoka mikononi mwa kundi la wananchi hao na kumpeleka kituo kikuu cha
polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani.
PICHA KWA HISANI YA GUMZO LA JIJI



No comments:
Post a Comment