Mkurugenzi, na mwanamuziki wa East African Melody Modern Taarab, Lamania
Shaaban amefarika usiku wa kuamkia leo akiwa usingizini. Lamania
alikuwa mpiga gitaa na mtunzi mzuri wa muziki wa Taarab, na atakumbukwa
kwa tungo zake kama 'Utalijua Jiji'.
Marehemu alianza kuugua kiasai cha miaka minne iliyopita baada ya kupata stroke iliyomuweka kitandani kwa muda mrefu sana, karibuni alianza kuwa na nafuu kiasi cha kuweza kuhudhuria Ibada kwenye Msikiti uliokuwa karibu na kwake. Lakini Mungu amempenda zaidi na amefariki leo.
Marehemu atazikwa Tandika Maguruwe, baada ya Ibada za mwisho katika Msikiti wa Sheikh Kilembe kesho saa 7 mchana. Msiba uko Tandika Maguruwe, Mtaa wa Muwale.

CHANZO: SANAA NA WASANII TANZANIA

No comments:
Post a Comment