
Mahakama Kuu ya Tanzania mchana huu imeweka wazi masharti ya dhamana
ya msanii wa filamu anayejulikana zaidi kwa jina la Lulu,. Lulu ambaye
jina lake halisi ni Elizabeth Michael anakabiliwa na mashtaka ya kuua
bila kukusudia ya msanii mwenzake(ambaye inasemekana walikuwa na
mahusiano ya kimapenzi), Steven Charles Kanumba, kilichotokea April
mwaka jana huko Sinza-Vatican jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo mahakamani mchana huu, dhamana ya mwigizaji Lulu ipo wazi endapo tu atatimiza masharti aliyotengewa ambayo ni
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo mahakamani mchana huu, dhamana ya mwigizaji Lulu ipo wazi endapo tu atatimiza masharti aliyotengewa ambayo ni
- Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
- Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
- Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
- Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania. Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba watumishi wawili wa serikali(Mahakama) ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama hawakuwepo.
Kwa maana hiyo, uwezekano ni wazi kabisa kwamba Lulu ataachiwa rasmi kesho January 29, 2013.PICHA NA MZEE WA MATUKIO DAIMA
No comments:
Post a Comment