Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake,
ukiingiwa kwenye eneo la Uwanja wa Ndege wa Kigoma uliopo eneo la
Kipampa, kwa ajili ya kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi
mkubwa wa kiwanja hicho unaoendelea ili kukiongezea uwezo.
Mafundi wa kampuni ya Resident Engineer inayokarabati uwanja huo wakiwa
kazini wakati msafara wa Kinana unakagua uwanja huo leo jioni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wafanyakazi kwenye uwanja huo alipowasili.
Meneja wa Uwanja huo, Elipind Tesha (kulia) akimweleza Kinana na ujumbe
wake hatua ilipofikiwa katika ujenzi huu, ambapo alisema, umefikia
asilimia tisini, na kwamba unaweza ingawa unaweza kuanza kutumika rasmi
Aprili mwaka huu, lakini matengenezo yote yatakuwa yamekamilika Juni
2013. Wengine kutoka kushgoto ni, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martin Shigela.
Kazi ya kupanua Uwanja ikiendelea
Msafara wa wanachama wa CCM wakipita kwenye eneo la matengenezo makubwa yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
Nape akiendesha moja ya vijiko vinavyotumika kufanya kazi
kwenye ujenzi huo. Alibeba mapipa ya lami kwa kutumia kijiko hicho na
kukiendesha kuyatoka eneo moja kwenda lingine.
Kinana akimsikilliza Mhandisi Mkazi wa Uwanja huo,Cleopa Mpembeni
(wapili kulia) akimpa maelezo ya kiufundi kuhusu ujenzi unavyoendelea.
Msafara ukitoka baada ya ukaguzi huo, Kinana akizungumza na wananchi wa Kigoma na Watanzania kwa jumla kuzitumia fursa za
kibiashara zitakazopatikana kutokana na kuboreshwa kwa Uwanja huo.
Picha zote na Bashir Nkoromo.
No comments:
Post a Comment