LULU APATA DHAMANA RASMI LEO KWA MILLION 40

 Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililomleta leo Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha taratibu za kupata dhamana.
Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na Askari Magereza
Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
Lulu akiingia mahakamani.
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliotala kufanya nae mahojiano mfupi baada ya kupata dhamana.
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari waliokusanyika mahakamani hapo.
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.
Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'
Lulu akiondoka mahakama hapo.
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi.  Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
 Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.
 Lulu akitokwa na machozi ya furaha
Lulu akiingia kwenye gari
---
Baada ya jana kushindikana kwa sababu zisizo zuilika hatimaye msanii maarufu Elizbeth 'Lulu' Michael ametoka kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yote ya dhamana yake yaliyo tolewa na mahakama kuu.

Mara baada yakutoka Lulu alieyeonekana akiwa mwenye majonizi na furaha kiasi aliomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado inaendela. Ali washukuru watu wote waliokuwa pamoja nae katika mkasa huuu  amabao bado unamzunguka na pia alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa pamoja nae katika kipindi chote cha matatizo yanayo mkabili

Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.
 
 Picha na Habari Mseto Blog

No comments

Powered by Blogger.