HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAANDAMANO KUHUSU GESI,PROF.MHONGO AJIBU MAPIGO.

 
PROFESA MUHONGO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA
MAANDAMANO YALIYOFANYWA MKOANI MTWARA HIVI KARIBUNI KUPINGA UWEKWAJI WA
BOMBA LA KUSAIRISHA GESI TOKA MTWARA HADI DAR ES SALAAM KWA MADAI GESI HAITAWANUFAISHA WAKAZI
WA MTWARA NA LINDI.
………………………………………………….
Watanzania wametakiwa kuacha mawazo potofu juu ya mgawanyo wa rasilimali
zilipo nchini kwa sababu zinatumika kwa ajili ya wananchi wote pasipoupendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Mhongo
wakati akitoa ufafanuzi kufuatia maandamano yaliyofanyika mkoani Mtwara kwa

madai kuwa ya gesi inayochimbwa mkoani humo kutowanufaisha wananchi wa

mikoa  ya Lindi na Mtwara.
Profesa Mhongo amesema maandamano kama hayo yanaweza kuligawa taifa kwa
sababu kila mkoa unatoa rasilimali zake ambazo zinatumika na wananchi wa

mikoa yote  bila kujali ukanda wa mikoa husika.
Waziri huyo amesema endapo wananchi  wa kila mkoa wataandamana ni hatari
kwa amani na utulivu na ustawi wa wananchi.
Waziri Mhongo amewataka wanasiasa wanatakiwa kuangalia maslahi ya kiuchumi
kwa Taifa badala ya kuwapotosha wananchi na kusababisha mivutano  isiyokuwa

ya lazima katika jamii.
Serikali imesema kuwa gesi asilia iliyogunduliwa Mtwara imekuwa ikitumika
kuzalisha umeme wa megawati 18 ambapo mikoa ya Lindi na Mtwara hutumia

kiasi cha Megawati 12 pekee.
Profesa Mhongo amesema serikali inaamini ujenzi wa bomba la gesi asilia
kutoka Mnazi Bay mpaka jijini Dar es Salaam utalinufaisha zaidi taifa kwa
kutumiwa katika viwanda,taasisi na matumizi ya kawaida majumbani.

PICHA NA FULL SHANGWE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: