Wananchi wakivuka kwa miguu katika Daraja la Manung’una, lililopo katika
Kijiji cha Msisi, Singida ambalo limekatika kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha. Picha Gasper Andrew
MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Singida,
zimesababisha maafa makubwa baada ya watu wawili, mmoja akiwa raia ya
China, kufariki dunia kwa kusombwa na maji, huku mamia ya abiria
wakikwama njiani baada ya daraja linalounganisha mkoa huo na mingine
kukatika.
Kukatika kwa Daraja la Munung’una kwa siku mbili
sasa, kumesababisha msongamano mkubwa wa magari yanayokadiriwa kuwa
zaidi ya 300.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa
waliofariki dunia kutokana na mvua hizo ni Xue Hui (36), maarufu kwa
jina la Kevin na Mariamu Samweli (18), mkazi wa Kijiji cha Maluga ambao
walifariki dunia kwa nyakati tofauti baada ya kusombwa na maji.
Vifo vyao vimeongeza idadi ya watu waliofariki
dunia kutokana na mvua mkoani Singida kufikia sita katika siku tatu
zilizopita. Mvua za juzi, zilisababisha watu wanne wa familia moja
katika Wilaya ya Mkalama kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba
ya tembe.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alisema raia
huyo wa China, alifariki dunia juzi jioni katika Kijiji cha Gumanga
Wilaya ya Mkalama baada ya gari alilokuwa anasafiria kusombwa na maji...
“Mchina huo alikuwa na mtoto wake ambaye alinusurika kifo.”
Alisema Mariamu alifariki dunia baada ya kusombwa na maji katika Mto Kiula uliopo katika Kijiji cha Igonia. “Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida.”
Alisema Mariamu alifariki dunia baada ya kusombwa na maji katika Mto Kiula uliopo katika Kijiji cha Igonia. “Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida.”
Mvua hizo kubwa zilizonyesha tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, zilisababisha daraja hilo la Munung’una lililopo katika Kijiji cha Msisi wilayani Singida kuvunjika.
Kutokana na athari hiyo, kumekuwa na msongamano mkubwa wa magari baada ya mawasiliano kati ya Singida na mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani kukatika.
Baadhi ya wananchi walilalamikia uharibifu huo
wakisema umetokana na ujenzi wa daraja hilo kuwa wa kiwango cha chini.
Dereva, George Medadi akitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam, alisema
daraja hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya kiwango.
Dereva mwingine, Iddi Mussa alisema barabara
nyingi zinazojengwa zimekuwa hazisimamiwi ipasavyo, kitendo
kinachochangia kuharibika haraka na kuisababishia Serikali hasara kubwa.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads),
Mkoa wa Singida, Mhandisi Yustaki Kangole alisema wamekubaliana na
Kampuni ya Ujenzi ya Chico kutoka China ambayo ndiyo iliyojenga barabara
hiyo kufukia shimo lililokata daraja hilo kwa vifusi vya mawe makubwa
ili iendelee kutumika mapema iwezekanavyo.
“Kwa sasa tunafanya kazi hii ya muda na baada ya
eneo hili kukauka, ndipo ukarabati mkubwa utafanywa ili kuimarisha
barabara hii muhimu kwa uchumi wa taifa,” alisema.
Mhandisi Kangole alisema Chico ilijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na kuikabidhi kwa Serikali mwaka 2008.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi alisema
kutokana na eneo hilo kufurika watu na mali, wameimarisha ulinzi na
kufungua kituo kidogo cha kutolea huduma za afya na kudhibiti uwezekano
wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.“Pia tumefungua Barabara ya Singida- Ndago Misigiri kwa ajili ya
kutumiwa na mabasi ya abiria na yale yenye uzito wa chini ya tani 10.
Vilevile tunaangalia uwezekano wa kuangalia ni namna gani watu
waliokwama, wanapata chakula,” alisema.
MWANANCHI
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment