Mkuu wa majeshi ya polisi,IGP Said Mwema.
Hata hivyo kichwa pamoja na mguu huo ulikutwa eneo
la tukio sambamba na kiwiliwili hicho, huku wananchi wengi wakiamini
kuwa kilichomuua ni kitendo cha baba yake kufa na kuacha mali kadhaa
ambazo mrithi mkubwa ni kijana huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
aliwaambia waandishi wa habari kuwa mauaji hayo yaligunduliwa Ijumaa
iliyopita baada ya kuokotwa kwa mwili wa kijana huyo chini ya daraja.
Mwili wa kijana huyo, Emannuel Vicent Chuwa (25)
ambao ulishaanza kuharibika ulikutwa chini ya daraja linalounganisha
Vijiji vya Kibosho Singa na Kibosho Sungu vilivyopo Wilaya ya Moshi
Vijijini.
“Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu
wanasema kijana huyo aliyekuwa akilelewa na baba yake mdogo alikuwa
haonekani kwa siku tisa mfululizo hadi mwili wake ulipopatikana,”
alisema Boaz.
Baba mzazi wa kijana huyo ni marehemu na alipofariki alimwachia urithi wa mali nyingi kijana huyo.
Kamanda Boaz alisema polisi wameanzisha uchunguzi
kuhusiana na tukio hilo la kinyama na inawashikilia baba mdogo na mama
mdogo ambao waliachiwa wosia wa kumlea marehemu huyo.
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment