Mwenyekiti
wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika
mkutano na uongozi wa NCCR-Mageuzi uliofika ofisi za Tume kuwasilisha
maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatatu, Jan 7, 2013)
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid na
kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.
Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi Ndg. James Mbatia akiongea katika mkutano na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba wakati chama chake kilipokwenda katika ofisi za
Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) kuwasilisha maoni
ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji
Joseph Warioba na katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid.
Baadhi
ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wakifuatilia mkutano kati ya chama chao na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013) wakati chama
hicho kilipowasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya.
Rais
wa Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA) Ndg. John Chipaka
akimkabidhi Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ndg. Mwatumu Malale
maoni ya chama chake kuhusu katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar
es Salaam leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013).
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ndg. Mwatumu Malale akiongea na uongozi
wa Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA) chini ya Rais wake
Ndg. John Chipaka wakati chama hicho kiliwasilisha maoni yake kuhusu
Katiba Mpya jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013).(Picha na
Tume ya Katiba).
Na Mwandishi Wetu
Tume ya Mabadiliko ya
Katiba leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013) imeanza mikutano ya ndani ya
kukusanya maoni ya makundi, vyama, asasi na taasisi mbalimbali kuhusu
Katiba Mpya.
Mikutano hiyo inafanyika jijini Dar es Salaam katika Ofisi za Tume hiyo na ukumbi wa Karimjee.
Kwa siku ya leo (Jan. 7, 2013), Tume ilikutana na vyama saba (07) vya siasa ambavyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM); Chama cha Wananchi (CUF); Chama cha NCCR-Mageuzi; Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Tanzania labour (TLP); Chama cha United Democratic (UDP) na Chama cha Tanzania Democtratic Alliance (TADEA).
Katika mikutano hiyo, vyama hivyo viliwasilisha maoni ya vyama vyao kwa maandishi na kuzungumza na baadae wajumbe wa Tume walipata fursa ya kujadiliana na viongozi wa vyama hivyo kuhusu masuala mbalimbali.
Mikutano hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho (Jumanne, Jan 8, 2013). Mikutano hiyo ya Tume na makundi mbalimbali inatarajiwa kumalizika tarehe 25 Januari mwaka huu (2013). Baada ya mikutano hiyo, Tume itafanya uchambuzi na baadae kuandaa rasimu ya Katiba itakayochapishwa katika magazeti mbalimbali na baadae kuwasilishwa katika Mabaraza ya Katiba nchini kote mwezi Juni, mwaka huu (2013).

Shukrani kwa Mo Blog

No comments:
Post a Comment