Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wakazi wa Igunga
Rais Jakaay Mrisho Kikwete akihutumia mamia ya wananchi wa Igunga
katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja wa Barafu mjini
Igunga baada ya kuzindua ujenzi wa daraja la Ndutu pamoja na mradi
mkubwa wa maji utaohudumia asilimia 70 ya wakazi wa Igunga.
Maelfu ya wakazi wa Igunga wakimsikiliza Rais Kikwete
| Rais Kikwete akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa Chujio la maji safi
kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa mji huo
watapata maji safi
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akijiunga na bendi ya Msondo
Ngoma kutumbuiza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa daraja la Mbutu la
Igunga
Wananchi wakivuka katika sehemu itayojengwa darala la kisasa la
Mbutu la Igunga ambao ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, hatua ambayo itatatua kabisa tatizo la miundombinu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la
vijana 10 ambao baada ya kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda
kikundi cha ujasiriamali mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo
Rais Kikwete akiangalia michoro ya Daraja litakalojengwa.











No comments:
Post a Comment