Marehemu Sadick Juma Kilowoko (Sajuki)
“MUME wangu amefariki dunia.” Haya ni maneno ya
Wastara Juma, mke wa Sadick Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki,
aliyefariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
jijini Dar es Salaam.
Baada ya maneno hayo aliyoyatuma kwa mwandishi wa
habari hii kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, Wastara
hakupokea simu yake iliyokuwa ikiita mara kadhaa kutaka ufafanuzi zaidi.
Sajuki ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea
kubeba jukumu la kugharimia matibabu yake, alifariki dunia jana
alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa kwa matibabu.
Alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, akisubiri kusafiri kwenda India kwa mara nyingine, kuendelea na matibabu
Alikuwa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, akisubiri kusafiri kwenda India kwa mara nyingine, kuendelea na matibabu
Alianguka jukwaani
Kabla ya kulazwaDesemba 18 mwaka jana, Sajuki alifikishwa hospitalini hapo akitokea jijini Arusha, baada ya kuanguka jukwaani kutokana na kuishiwa nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika, ili kumtazama katika Tamasha la Asante Tanzania.
Tukio hilo lilitokea katika tamasha hilo
lililohusisha wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya
lililofanyika ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, wakati msanii huyo
alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Baada ya kupandishwa jukwaani, alipewa kipaza
sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida
alifanikiwa kutamka neno moja tu,”ahhh” na kisha kudondoka akiwa juu
ya jukwaa na kabla ya kutua chini, alidakwa na wasanii wenzake
waliokuwa pembeni,”
Wasanii hao walimshusha jukwaani baada ya kumpumzisha kwa muda na kumtaka aende kupumzika zaidi. Akihojiwa baada ya tukio hilo, Sajuki alisema kwa sauti ya upole kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu. ”Hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana, sijisikii vizuri,”alisema Sajuki.

Haya ni maneno ya mwisho ya Sajuki kwa vyombo vya
habari, wakati akiwa tayari amepitiliza siku zake za kurudi India,
kuendelea na matibabu yake baada ya kukosa Sh28 milioni.
Wastara aliwahi kumwambia mwandishi wa habari hii
kuwa, Sajuki alipaswa kurejea India Desemba 6 mwaka jana, lakini
alikwama kufanya hivyo kutokana na upungufu wa pesa. Hata hivyo
alisema waliamua kuandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kutunisha
mfuko wa matibabu yake.
Tamasha la kwanza la wasanii hao lilifanyika
mkoani Iringa Novemba 25 mwaka jana na kupambwa na wasanii wengi wa
muziki na filamu. Tamasha lingine lilifanyika Desemba 18 jijini Arusha.
Ugonjwa wa Sajuki
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu, yalipamba moto.
Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe
pembeni ya ini, mapema mwaka 2011 alipoanza kuugua. Mei mwaka 2012
alifanikiwa kwenda India kwa matibabu na baadaye alirejea nchini na
kuonekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Waongoza Filamu
wa Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri, hivi karibuni, Sajuki alikuwa
anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu, uti wa mgongo na kansa ya
ngozi.
Mikasa
Sajuki ambaye ameacha mjane ‘Wastara’ aliye mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa yao, alikumbwa na mikasa mingi jambo lililosababisha kutokufanya sanaa yake ya uigizaji kwa ufanisi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
MWANANCHI
Alipokuwa India kwa matibabu, Sajuki aligundulika kuwa ana ugonjwa mwingine, tofauti na ule uliompeleka kufanyiwa upasuaji.
Kwa mujibu wa Wastara, walipokuwa India (katika
Hospitali ya Apollo), Sajuki alifanyiwa vipimo mbalimbali ili kubaini
matatizo yanayomsumbua.
Alisema katika uchunguzi huo, ilibainika kuwa mumewe alikuwa na tatizo kwenye uti wa mgongo na ngozi ya mwili mzima.
Alisema katika uchunguzi huo, ilibainika kuwa mumewe alikuwa na tatizo kwenye uti wa mgongo na ngozi ya mwili mzima.
Baadaye pia ilibainika kuwa alikuwa na tatizo la
pumzi, jambo lililosababisha asitibiwe ugonjwa wake ambao kabla ya
kufanyiwa operesheni, alitakiwa kuwa katika hali ya kawaida.
Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na kufikia kipindi
cha kudhoofu mwili jambo lililosababisha wasanii wenzake na watu
wengine, kuamua kumchangia fedha ili akapate matibabu.
Wasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi hilo na kumwezesha kwenda India kwa mara ya kwanza Mei mwaka 2012.
Wasanii, wanasiasa, wananchi walifanikisha zoezi hilo na kumwezesha kwenda India kwa mara ya kwanza Mei mwaka 2012.
Hata hivyo alikuwa hajapona sawasawa na alikuwa
anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi na hili alilikiri kwenye
kipindi cha ‘Mkasi’ kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.
Mikasa
Sajuki ambaye ameacha mjane ‘Wastara’ aliye mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa yao, alikumbwa na mikasa mingi jambo lililosababisha kutokufanya sanaa yake ya uigizaji kwa ufanisi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
Sajuki na Wastara walipata ajali hiyo katika
maeneo ya Tabata Bima, ajali iliyosababisha Wastara kupoteza mguu wake
mmoja. Hata hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa
ameshapeleka posa kwa familia ya kina Wastara.
Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanamume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.
Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanamume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.
MWANANCHI

No comments:
Post a Comment