Serikali
inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba mchakato wa maandalizi
ya kutungwa kwa Sheria ya Kusimamia Vyombo vya Habari (Media Services Bill) upo katika ngazi za juu Serikalini.
Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakati wowote baada ya kupitishwa katika ngazi za juu za Serikali.
Mswada unaotarajiwa kuwasilishwa
ni ahadi ya Serikali tangu mwaka 2007. Serikali ipo tayari kupokea
hoja mbalimbali baada ya kuwasilisha mswada huu Bungeni kwa maana ya
kuboresha ikiwemo Haki ya Kupata Habari.
Serikali inawataka wadau wa
habari na watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuhakikisha
kwamba Mswada wa Kusimamia vyombo vya Habari unakamilika na kuwa sheria
lengo likiwa ni kujenga misingi ya demokrasia na utawala bora.
24/1/2013
No comments:
Post a Comment