Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU) akiangali Jengo la PPF
Tower baada ya kuzima moto uliounguza sehemu ya juu ya jengo hilo,
jijinii Dar es Salaam jana.
Picha na Salhim Shao
Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika, unadaiwa kuzuka katika ghorofa hiyo ambako kuna ofisi za Abbot Fund na Seven Seas.
Waandishi wa habari hizi waliofika kwenye jengo
hilo saa 3:00 asubuhi, walishuhudia moshi mkubwa ukifuka kutoka sehemu
ya juu ya jengo hilo, ambako ipo mitambo ya mawasiliano na vifaa
vingine.
Moshi huo ambao unadaiwa kuanza kuonekana tangu
mapema alfajiri, uliendelea hadi muda huo na magari ya vikosi mbalimbali
vya zimamoto yalifika eneo hilo na kuanza jitihada za kuzima moto huo.
Magari hayo licha ya kupata maji kwa ajili ya kuzimia moto huo, kutokana
na moshi uliokuwa umetanda katika jengo hilo kuanzia ghorofa ya 17
ulifanya washindwe kufika kwenye chanzo.
Waandishi walishuhudia watu watatu wakiwamo
walinzi wa Kampuni ya KK Security wakiwa wamekwama sehemu ya juu ya
jengo hilo, kutokana na ngazi za kushukia kukumbwa na moshi mzito.
Hata hivyo, saa 4:30 aubuhi baadhi ya askari wa
Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiwamo wale wa kampuni binafsi waliweza
kuwafikia watu hao na kuzima moto ambao ulikuwa unawaka eneo la juu la
jengo.
Kaimu Kamishna wa Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto,
Pius Nyambacha alisema walifika kwa wakati eneo la tukio na kwamba,
miundombinu ya maji kwa ajili ya kuzimia moto iliyopo jengo hilo
ilisaidia kufanikisha uzimaji huo.
Nyambacha alisema ni mapema kujua chanzo cha moto,
lakini la msingi umethibitiwa na aliwataka wanaojenga majengo marefu
kuzingantia uwekaji miundombinu ya moto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik alisema miundombinu thabiti ya maji ya kuzimia moto katika jengo hilo, ndiyo iliyookoa hasara zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik alisema miundombinu thabiti ya maji ya kuzimia moto katika jengo hilo, ndiyo iliyookoa hasara zaidi.
“Wamejitahidi sana PPF kwani kila ghorofa lina miundombinu ya maji ya kuzimia moto, hali ambayo ilisaidia kuudhibiti,” alisema.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment