Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali.
Fina Mango akipiga picha na Halima Mdee wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Makutano.
Mbunge
wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule
za binafsi maarufu kama “Academia” inachangia matokeo mabovu ya kidato
cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali
la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati
akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano.
“Kwa
Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule
hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa
ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa
kutoa maelekezo unakuwa haupo” .
Mdee
aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali
iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au
kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango
wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.
(MMES
II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha
ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango
kipande hadi 70% lakini ilipofika 2009 kiwango cha ufaulu kikashuka
hadi 17%, 2011 kikashuka tena hadi 9% na mwaka jana kikazidi kudidimia
mpaka 5%.
Mdee
alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalozikabili shule za kata ni
miundombinu ya shule na maslahi ya walimu kwa kusema “Kinachojitekeza
sasa ni mrundikano wa frustration za walimu, wamekata tamaa kabisa kwa
sababu vipato vyao ni vidogo sana, lakini pamoja na kuwa vidogo vile
wanavyotakiwa kuvipata kutokana na vipato kuwa vidogo hawavipati , na
zaidi wakati walimu wanasema wanadai serikali inasema hawadai”.
Mheshimiwa
Halima Mdee alimalizia kwa kusema anadhani ni wakati sasa kama taifa
lazima serikali iamue inataka kufikisha wapi elimu kwa kuwepo bajeti
inayotosheleza mahitaji na kuzingatia hali halisi ya maisha na soko, na
kusisitiza uwepo wa mitaala inayoeleweka tofauti na hivi sasa ambapo
waalimu wanasema wanapokea maelezo tu na kujiandalia wenyewe mitaala.
Pia alisisitiza uwepo wa mgawanyo wa walimu bila upendeleo kwa kila
shule tofauti na sasa ambako kuna shule hazina walimu wa kutosha na pia
uwepo mamlaka ya usimamizi wa elimu yenye nguvu.
Mahojiano yote yanapatikana katika:




No comments:
Post a Comment