Hoteli ya
Hyatt Regency Kilimanjaro imeamua kuialika kampuni ya usafi ya Green
Waste Pro baada ya kuona juhudi zao za kuweka Manispaa ya Ilala safi na
mabadiliko yanaonekana ndipo wakaamua kushirikiana nao katika zoezi la
kusafisha fukwe hizo.
Wafanyakazi
wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green
Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya
hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo iliyojipangia kufanya
zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira.
Meneja
Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena
(kushoto) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Kivukoni
Front baada ya kupata mwaliko kutoka Hoteli ya Hyatt Regency wa
kushiriki katika kusafisha fukwe hizo.
Mwananchi
asiyefahamika akiwa amechapa usingizi huku akiwa amejifunika gunia chafu
na kulifanya kuwa shuka katika kichaka cha fukwe za Kivukoni Front
wakati zoezi la usafi likiendelea.WADAU huyu jamaa hatuna uhakika kama
naye ni sehemu ya uchafu au ndio nyumbani?? Tembea uone.
Picha juu
na chini ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro
wakiwa wamebeba mafurushi ya lundo la uchafu uliokusanywa kutoka kwenye
fukwe za Kivukoni Front zilizopo karibu na Hoteli hiyo.
Moja ya
magari ya kukusanya uchafu ya kampuni ya Green Waste Pro likiwa
limesheheni lundo la uchafu uliokusanywa toka kwenye Fukwe za Kivukoni
Front baada ya kusafishwa na Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa
kushirikiana na kampuni ya usafi ya Green Waste Pro.
Wafanyakazi
wa Hoteli ya Hyatt Regency na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green
Waste Pro ltd wakibadilishana mawazo baada ya kuhitimisha zoezi la
kusafisha fukwe za Kivukoni Front na kuishukuru kampuni ya Green Waste
Pro kwa kuitikia wito.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Hyatt Regency na kampuni ya Green Waste Pro baada ya zoezi la usafi.
PICHA NA FULL SHANGWE



No comments:
Post a Comment