Mkurugenzi
kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer
akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni
zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti
vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora 2013/14
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki
Jawad Jaffer akimkabidhi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya
MeTL Group Hussein Dewji cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa
kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Raha Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa Mwakilishi wa
Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa pili kulia)
wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa makampuni bora
kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia)
aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga (
wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na
thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji
akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Na.Mo Blog Team
Taasisi huru ya Superbrands
ambayo ni kubwa kuliko zote duniani, inayoratibu ubora na thamani ya
nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji, leo imekabidhi vyeti
vinavyotambuliwa kimataifa vya utambuzi wa ubora wa bidhaa kwa kampuni
zilizofanya vizuri nchini Tanzania kwa mwaka 2013/2014.
Tuzo za Superbrands ni miongoni mwa tuzo zenye thamani kubwa na zinazoleta heshima ya pekee ndani ya kampuni.
Hii ni mara ya tatu kwa tuzo
hizo kutolewa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake
yapata miaka mine iliyopita.
Uamuzi na hatimaye utoaji wa
tuzo husika unatoka baraza huru la wataalamu waliobobea katika masuala
ya biashara, lakini lengo hasa likiwa ni ni kustawisha na kuhamasisha
ari katika utoaji huduma zinazo zingatia ubora.
MeTL imekuwa moja wapo kati ya Makampuni yaliyopokea vyeti vya tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya tatu hapa nchini.



No comments:
Post a Comment