WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda
Aliyasema hayo juzi alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha SOS Children’s Village kilichopo eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru, mkoani Arusha na kujionea hali halisi ya kituo hicho.
Alisema kumekuwapo na ongezeko kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaotokea katika maeneo mbalimbali hali ambayo imekuwa ikisababishwa na walezi ama wazazi wao kutokana na migogoro katika familia na kusababisha watoto wengi kutoroka nyumbani na kuishia mitaani.
Alisema kutokana na hali hiyo kumekuwapo na idadi kubwa ya watoto ambao wamekuwa wakilelewa katika vituo mbalimbali na kupatiwa huduma za kijamii.
Pinda katika kuona umuhimu wa kituo hicho pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili alichangia Sh60 milioni kusaidia kutatua changamoto mbalimbali kituoni hapo.
Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Modern
Holdings (EA) Limited Anselm Minja ambaye alimuunga mkono waziri mkuu
kwa kuchangia Sh10 milioni.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment