Rais Jakaya
Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa kuendelea na semina, leo kwenye
Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed
Shein na Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula
na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (PICHA ZOTE NA BASHIR
NKOROMO@Nkoromo Blog)
Mwenyekiti wa
CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha NEC kwa semina iliyoanza
jana, na kuendelea leo kwenye ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM,
mjini Dodoma. Pamoja naye ni Dk. Sheni na Kinana
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Uchumi
na Fedha Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.
Katibu Mkuu
wa CCM Abdulrahman Kinana akisahuriana jambo ukumbini na Katibu wa NEC
Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo
Mjumbe wa
NEC, Mama Salma Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC Siasa ana Uhusiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati
ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Wajumbe wa NEC Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika wakibadilishana mawazo ukumbini
Katibu wa
NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akichati
jambona Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye kabla ya kikao
Nape (kulia) akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Sitta
Katibu Mkuu
mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, William Mukama
akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC Profesa Juma Kapuya
ukumbini
Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na kuweka kumbukumbu ya mijadala inayozungumzwa kwenye mkutano huo
HII UNAONAJE? Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiteta jambo na Mzee Mtandika
Dk. Asha-Rose Migiro na Nape katika mazungumzo yao ukumbi kabla ya
kikao
HAPO VIPI?
Katibu wa Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib anaonekana kumuuliza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati wakibadilishana
mawazo kabla ya kikao kuanza
Wajumbe wakisubiri kwa hamu kikao kuanza
Makamu wa
Rais Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda
wakiwa safu ya mbele na baadhi ya wajumbe kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kikao kuanza
Aliyekuwa
Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma aka Mama Mshua (kulia)
akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabiba
nje ya ukumbi. Katikati ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba
ENZI ZETU ZA
IGUNGA VIPI? Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba anaonekana
kumuuliza swali hilo Mjumbe wa NEC, aliyekuwa mbunge wa Igunga Dk.
Dalaly Kafumu walipokutana nje ya ukumbi kabla ya kikao kuanza
CCM MAMBO SAFI TU! Mukama akimwambia Mjumbe wa NEC, Steven Wasira nje ya ukumbi
Wajumbe wa
NEC wakiangua kicheko cha kutaniana kaba la kuingia ukumbini. Kutoka
kulia ni Dk. Rafael Chegeni, Januari Makamba, Halimenshi Mayonga na
Samwel Sitta
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment