Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, Ndugu Sadifah Juma
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamisi amemvua ujumbe wa Baraza la Umoja huo Taifa aliyekuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paul Makonda kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamisi amemvua ujumbe wa Baraza la Umoja huo Taifa aliyekuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paul Makonda kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha baraza kuu la
UVCCM zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa Makonda alifukuzwa
muda mfupi baada ya kufungulia kwa kikao hicho kinachoendelea mjini
hapa.
Chanzo chetu kilieleza kuwa mara baada ya kuanza
kikao hicho, Mwenyekiti alimwita Makonda na aliposimama alimweleza mbele
ya wajumbe kuwa amemfuta ujumbe wa Baraza.
“Nimekuvua ujumbe kuanzia sasa kwani haiwezekani
taarifa za chama ukazianika kwenye vyombo vya habari,” alilalamika
mwenyekiti huyo.
Mapema asubuhi jana, Sadifa aliwaonya wajumbe kuwa
asingekuwa na msalia mtume kwa watu ambao wanafanya shughuli za chama
kinyume na matakwa kamili ikiwamo kuchanganya mapenzi na kazi za chama.
Alipotakiwa kuthibitisha kufukuzwa kwake Makonda
alikiri kuwa alikuwa amefukuzwa na Mwenyekiti lakini akakataa kufafanua
sakata hilo.
“Mimi ninachojua ni kuwa mwenye haki akionewa,
mbingu husimama nyuma yake! Kama ni kufukuzuzwa ni kweli nimefukuzwa
bila ya kujua sababu kamili,” alilalamika Makonda. Hata hivyo taarifa
zilidokeza kuwa siku tatu kabla ya kikao hicho, alipigiwa simu na
Mwenyekiti na kutakiwa ahudhurie kikao hicho.
Inaelezwa kuwa alipoingia kwenye kikao alifanya
usajili kama wengine na kupewa posho pamoja na nyaraka za kikao hicho
zinazofafanua juu ya ajenda.Taarifa za kuaminika zilieleza kuwa mara
baada ya kupewa taarifa za kufukuzwa, mjumbe huyo alirudisha kwa hiyari
yake makabrasha ya chama pamoja na posho zote kisha akaondoka eneo la
mkutano.
Mkakati wa Sadifa kutumia madaraka yake kuwaadhibu
wajumbe wenye tuhuma za kukiuka kanuni za UVCCM alianza kuzionyesha
wazi wakati akifungua kikao cha Baraza hilo alipoonya mtu yeyote
atakayekiuka maadili hatamwonea huruma.
Aliwaonya akisema hataona aibu kufanya hivyo hata kwa yule ambaye alikuwa akimfanyia ka mpeni zilizomwezesha kukalia kiti hicho.
“Sitavumilia upuuzi huo. Baada ya uchaguzi kupita
mimi ni Mwenyekiti wa Vijana wote ndani ya chama changu wa Tanzania bila
kujali kama walinichagua au hawakunichagua. Hivyo ninaomba tufanye kazi
kwa kushirikiana kwa pamoja,” alisema Sadifa.
“Hata kama ulinipigia kampeni wakati wa uchaguzi
mkuu ukifanya kosa nitakuwajibisha kama mtu mwingine yeyote na kamwe
sitapendelea mtu eti kwa sababu tu alinipigia kampeni. Huu ni wakati wa
kazi na wakati wa kazi tusicheke,” alionya.Mbali na hilo mwenyekiti huyo
aliwatahadharisha viongozi wa jumuiya hiyo kujiepusha na vitendo vya
kuchanganya kazi na mapenzi kwa madai kuwa vinazorotesha uwajibikaji
ndani ya chama.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mboni Mhita, aliwataka
wanachama wa UVCCM kuachana na siasa za chuki na majungu kwani hazina
nafasi katika jumuiya hiyo.
Aliwataka vijana kujitolea kwenye kazi za kijamii
kwani ndiyo iliyowaweka madarakani na kuachana na mambo yao binafsi
kwenye vikao na badala yake washirikiane kikamilifu na jamii
inayowazunguka.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment