Mama huyo akimdhibiti mwizi huyo
Shughuli ya kumdhibiti ikiendelea.
Mama huyo akiendelea kumdhibiti jamaa huyo kwa kumpiga tanganyika jeki.
Jamaa huyo naye akigeuka mbogo huku akijaribu kujitetea na kuwa mkali bila mafanikio.
Mama
ambaye hakuweza kufahamika mara moja jina lake, akimrushia konde zito
jamaa aliyedaiwa kumwibia mkoba wake mama huyo, uliokuwa na pesa, simu
pamoja na Paspoti ya kusafiria ya mumewe anayeonekana pichani (wa pili
kulia). Imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa amenasa katika kijimtaro eneo
la Kituo cha Samaki Mbezi Beach jana usiku majira ya saa nne, na kuamua
kuomba msaada wa kunasuliwa gari yake katika eneo hilo kutoka kwa
waendesha Pikipiki 'Boda Boda' waliokuwa wakisubiri abiria kituoni
hapo.
Imeelezwa
kuwa baada ya kuoba msaada walijitokeza vijana kutoka miongoni mwa
waendesha pikipiki hao na kumnasua mama huyo wakisaidiana na mumewe,
lakini baada tu ya kufanikisha zoezi hilo mmoja wao aliingiza mkono
katika dirisha la nyuma na kuchukua mkoba na kisha kuanza kukimbia nao
huku mume wa mama huyo akijitahidi kuwakimbiza bila mafanikio, huku
jamaa huyu aliyekamatwa akisikika kuwatetea jamaa hao, akisema, 'achana
nao hao mimi nawafahamu', ndipo mume wa mama huyo alipoamua kuruachana
nao kwani walivuka barabara na kutokomea goizani upande wa pili wa
barabara na kurudi kuanza kumuuliza vizuri jamaa huyo ili waweze kufanya
taratibu za kuwapata.
Ghafla
jamaa huyo alianza kukana kuwa hawafamu, ndipo songombingo ilipoanza
kwani mume na mke waliamua kumng'ang'ania jamaa huyo huku wakisaidia na
baadhi ya waendesha pikipiki waliokuwa eneo hilo hadi walipofanikiwa
kumpandisha katika gari yao na kuelekea naye kituoni.
No comments:
Post a Comment