Na John Banda, Manyoni.
FAMILIA 220 za wanachama wa chama cha
Wakulima wa Zao la Tumbaku wa kijiji cha
Msemembo wilayani manyoni mkoani Singida wazimeziacha nyumba zao na kukimbilia
mapolini kutokana na Chama cha ushirika cha Msemembo Amcos kuamua kumtumia
dalali wa kampuni ya Mwankoko Auction Mart Co.LTD ya mjini Singida.
Kukamata mali na nyumba za wakulima hao kwa madai kuwa wameshindwa kulipa madeni ya mikopo
ya fedha katika kipindi cha mwaka 2010/11 walizokopeshwa kwa ajili ya msimu wa
kilimo cha zao la tumbaku.
Wakizungumza kwa niaba ya wakulima wezao
Wilison Kingo na Shabani Sabuni wasema kampuni ambayo iliyotumiwa na ushirika huo ni
Mwankoko Auction Mart Co.Ltd ya mjini Singida ambayo inashirikiana na viongozi
wa ngazi ya juu wa chama cha ushirika wa
Msemembo Amcos kilichopo kijiji cha Msemembo
Wilaya ya Manyoni.
Kingo alisema kutokana kampuni hiyo ya udalali
ambayo waliambatana na Askari wa Jeshi
la Polisi waliobeba silaha za moto walipita nyumba hadi nyumba za wanachama na
kubadika matangazo yanayowataka wakulima hao kulipa madeni hayo kwa siku 14 zinazoishia Jan 8.2013
“Baada ya kuona kampuni hiyo ya udalali
wakiwa na askari wa polisi katika harakati za kuweka matangazo kwenye nyumba zao, walishikwa na hofu kubwa
na kulazimika kukimbilia maporini kwa hofu ya kufilisiwa nyumba zao na mali”alisema Kingo.
Wakizungumza
zaidi wanachama hao walisema viongozi
hao wametumia mbinu za kuwadharirisha baada ya kungundua kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha miongoni mwa na mali za
ushirika ili kuficha ukweli wa madeni
wanayodaiwa na kuamua kumtumia dalali na
polisi kuja kuweka matangazo ya kutaka kufilisi nyumba na mali zao.
Wakulima hao hata hivyo wamesikitishwa na
Diwani wa kata hiyo Msemembo Moses Matonya kwa kushindwa kulishughulikia suala
hilo lililosababisha wananchi wake kukimbilia maporini ambapo kwa upande wake
alimtaka dalali huyo kuhakikisha anakamata nyumba na mali za wanachama hao.
“Diwani huyo amekuwa akimsisitiza dalali wa
kampuni hiyo kuhakikisha anakamata mali na nyumba zetu bila kujali wakulima hao ambao wengi wao
wamekimbilia maporini na watoto wengine wakishindwa kwenda shuleni kwa hofu ya
kuuzwa nyumba na mali hizo”walisema .
Mapema mwezi wa Desemba 2012 Ofisi ya Mkuu wa wilaya ilipelekewa
taarifa kuhusu mgogoro huo kati ya viongozi wa ushirika na wanachama ambapo kwa
upande wake aligiza kusitishwa kwa zoezi hilo la dalali la kutaka kukamata
nyumba na mali zao.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Katibu
Tawala wa Wilaya ya Manyoni Paul Sinje alimtaka Mwenyekiti wa ushirika huo Amos
Lameck kufuata mambo yafuatayo yakiwemo ya
kusitisha zoezi hilo,kufanyika kwa mkutano wa wanachama na wakulima wa
zao hilo ili kufikia maamuzi ya pamoja.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya aliwataka viongozi
hao kufuatilia madeni kwa mujibu wa sheria na kanuni walizojiwekea, huku
akiagiza Orodha ya wakulima ambao wamelipa fedha bila ya kupewa risti iwasirishwe kwenye
ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
“Ofisi ya Wilaya Imebaini makosa uliyofanya
katika kufanya kazi hiyo, ita mkutano wa wanachama wote, fuata kanuni na
Sheria, Orodha ya waliolipa bila kupewa Risiti iletwe, pia utendaji kazi wa
Namna hiyo hautavumiliwa hata kidogo’’. Ilisema sehema ya Barua hiyo ya Tar 3
DES 2012 na Kusainiwa na Afsa Tarafa Paul Sinje
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ushirika wa
Chama cha wakulima wa tumbaku Lameck Amosi alisema kuwa wakulima hao wanadaiwa
kiasi cha shilingi zaidi ya million 60 kwa wanachama 108
Alisema kutokana na chama hicho kubanwa na
Benki kikitakiwa kulipa deni hilo uongozi wake uliamua kuileta kampuni hiyo ya Udalali
ili kuweza kukamata nyumba, mashamba na mali nyingine ili ziunzwe na kulipa deni hilo lakini siyo
kweli wanachama hao hivi sasa wamekimbilia maporini na Barua ya mkuu wa Wilaya.
“Madalali mali nyingi wanapokwenda kufilisi
mali ya watedaiwa walio wengi huenda na Polisi kwa ajili ya usalama hivyo
uongozi wa ushirika hauhusiki na ujio wa polisi hao na hata Barua ya kuitisha
mkutano siyo kweli”, alisema Amosi katika mahojiano kwa njia ya simu.
Mwisho.
HABARI KWA HISANI YA JOHN BANDA
No comments:
Post a Comment