Hii ndio hali halisi ya Alex baada ya kupigwa na maasikari baada ya kufanya biashara eneo ambalo sio sahihi.
Sehemu hii ya mguu alipigwa na singa (ncha ya bunduki kwa mbele) ambayo ilimtoboa mpaka ndani ya mguu wake.
Alex
Yona Machela ni mkazi wa Dodoma na pia ni mjasiliamali (chinga)
alipigwa tarehe 6/03/2013 mda wa saa 11:25 barabara ya Saba (One Way)
karibu na kitemba hoteli iliyoko Dodoma mjini. Alikuwa anafanya biashara
ya kuuza viatu. Sababu za kumpiga Chinga huyo ni kwa sababu sehemu
ambayo alikuwa anafanyia biashara sio sahihi.
Alipakiwa
kwenye gari la manicipal ya Dodoma akiwa salama ila alipofikishwa
ndani ya ofisi ya Manicipal maasikari walianza kumpiga Alex (Chinga) kwa
kutumia vitako vya bunduki na pia walimpiga kwa kutumia singa (ncha ya
bunduki kwa mbele) maeneo ta mguu wake na kuumia vibaya.
Pia
walitumia rungu kumpiga Alex kwenye miguu, mgongoni na mikononi bila
huruma hii yote ni kwa sababu ya kuuza viatu sehemu ambayo sio sahihi
hapa kweli kuna haki maana kama kweli amekosa ila sio kumpiga kama kibaka au mwizi
kwa hali kama hii polisi watasababisha kutoelewana kati ya raia wema na
wao maana hawana hata huruma kwa binadamu mwenzao na isitoshe ni
mtanzania mwenzao.
Pia
Alex (Chinga) alikuwa na viatu pear/ pics 120 ambazo mpaka sasa ziko
Manicipal ya Dodoma na pia Manicipal walifungua kesi kwa kudai kuwa Alex
Yona Machela alikwenda kumtetea muuza viatu ambaye alikuwa anauza viatu
eneo ambalo sio sahii ndipo maasikari walianza kumpiga kwani alikuwa
anawazuia wasifanye kazi yao.Kesi hii imefunguliwa mahakama ya mwanzo ya Chamwino iliyoko Dodoma mjini.
Kwa
maelezo ya Alex (Chinga) anasema baada ya kushikwa kwa kuuza viatu
sehemu ambayo hairuhusiwi alipandishwa kwenye gari akiwa na pear zake
120 za viatu ambazo maasikari walizishika wakaelekea municipal ya mji wa
Dodoma lakini baada ya kufikishwa ofisini maasikari walianza kumshushia
kipigo kwa kusema hii ni fundisho kwa wengine. Anaendelea kusema
alipigwa mpaka akapoteza fahamu.
Na
pia anasema kesi aliyofunguliwa na Manicipal sio ya kweli kwani viatu
ni vya kwake na wali sio vya mtu mwingine kama manicipal wanavyodai
kwani wanataka kujikinga kwa kusema uhongo ili kupoteza ukweli wa jambo na mali yake
ipotee kwa kutumia mgongo wa mahakama.Pia Alex anasema amefungua kesi
nyingine baada ya manicipal kufungua kesi ambayo inapotosha ukweli wote
ili usijulikane.
PAMOJAPURE BLOG





No comments:
Post a Comment