HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Majambazi wavamia ofisi za TCU, wapora mali

 
Kamanda Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
 
Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwa kushirikiana na mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Nge, wamevamia ofisi za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na kumlewesha kwa chakula kinachodaiwa  kuchanganywa na dawa za kulevya mlinzi wa kampuni anayelinda katika ofisi hizo na kuvunja milango kisha kupora nyaraka na mali mbalimbali.
 
Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa  lilitokea usiku wa kumkia jana. Alivitaja vitu vilivyoibwa kuwa ni kompyuta tano, Laptop mbili  pamoja na CPU moja vyenye thamani ya Sh milioni 14.
 
Alisema  walinzi wawili wa kampuni ya ulinzi ya Nge, Said Abdalah na Kasimu Salehe  walikuwa zamu ya kulinda katika ofisi hizo. Alisema  ilipofika nyakati za usiku Said alimpa mwenzake chakula kinachosadikiwa kuchanganywa na jana asubuhi alikutwa akiwa amelaa bila kujitambua.
 
Kamanda Kenyela alisema baada ya mlinzi huyo kufanya kitendo hicho, alitoroka.
 
NIPASHE lilifika eneo la la tukio na kushuhudia baaddhi ya milango ikiwa imevunjwa kwa vitu vizito. Pia kabati la kuhifadhia nyaraka muhimu lilikatwa kwa kutumia moto wa gesi huku ofisi zingine zikiwa zimepekuliwa na nyaraka kutupwa ovyo.
 
Taarifa zinaeleza kuwa mlinzi aliyempa mwenzake chakula hicho kinachosadikiwa kuwa na dawa za kulevya aliajiriwa Februari 26, mwaka huu na hafahamiki anakoishi.
 Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Nge, Pius Mgaya, alisema  waliingia mkataba ya ulinzi na TCU Machi 1, mwaka huu.
 
Alisema mlinzi wao aliyekimbia baada ya kufanya kitendo hicho alidhamilia kwa muda mrefu kutokana na baada ya tukio hilo alibadilisha nguo za kazi na kuvaa za kiraia pamoja na kuacha bunduki ikiwa na risasi tano. Afisa Habari wa TCU, Edward Mkaku, alisema ofisi saba zilivunjwa na baadhi ya vitu zikiwamo kompyuta kuchukuliwa. 
 
Alisema kutokana na tukio hilo, kuna haja TCU kuweka  mitambo ya kuhifadhi matukio yote yanayotokea katika taasisi hiyo kwa sababu ni tukio la pili TCU kuvamiwa inavamiwa na majambazi katika kipindi cha mwaka mmoja. Juni 25, mwaka jana ofisi hizo zilivamiwa na kuporwa vitu mbalimbali zikiwamo fedha na kompyuta
 
 
CHANZO: NIPASHE

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: