Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo
za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na kusherehekea siku ya
Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, .
Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa kwanza
wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume, wakati wa hafla ya utoaji
tuzo hizo iliyofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake
Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Picha
na OMR).
Picha juu
na chini ni Washiriki wa onyesho la mitindo ya mavazi ya Mwanamakuka,
wakipita jukwaani wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi
wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, ambapo zawadi hizo zilikabidhiwa na Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mama Asha
Bilal, akishiriki pamoja na wageni waalikwa kuburudika kucheza muziki wa
kizazi kipya wa Msanii Q-Chilla, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za
Mwanamakuka zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Mwanamke
Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, na
baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa muziki
wa kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya
kutoa tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku
ya Wanawake Duniani, katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam
Mke wa
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Wadhamini waliofanikisha kufanyika kwa
hafla hiyo ya utoaji tuzi za Mwanamakuka 2013, baada ya kukabidhi tuzo
hizo kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.



No comments:
Post a Comment