Afisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya akifanya kazi ya
kuhesabu kura zilizowasilishwa katika kituo cha kuhesabu kura mjini
Nairobi. Picha na AFP
Jana mashirika ya kijamii yalikwenda
mahakamani kufungua kesi ili kuitaka Mahakama Kuu kusitisha shughuli
inayoendelea ya kuhesabu kura.
Mahakama Kuu ilitakiwa kutoa uamuzi wa kesi
hiyo na mashirika hayo ya kijamii, ambayo pia yanashinikiza zoezi
linaloendelea la kuhesabu kura za urais katika Ukumbi wa Bomas
kusitishwa.
Makundi hayo yalidai kuwa IECB inakwenda
kinyume na Katiba ya Kenya inayoelekeza kwamba kura kuhesabiwa kwa njia
ya elektroniki.
Kufuatia kesi hiyo, majaji watatu waliteuliwa kuisikiliza ambao ni Jaji Isaac Lenaola, Jaji David Majanja na Jaji Weldon Korir.
Hata hivyo, majaji hao walisema kwamba mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Wakati makundi hayo yakichukua hatua hiyo,
tume hiyo ya uchaguzi nayo ilisema kuwa idadi kubwa ya kura
zilizoharibika zilitokana na hitilafu katika mtambo wake, ambao ulikuwa
ukiongeza idadi ya kura hizo mara nane.
Wakati hayo yakiendelea, hadi sasa matokeo
ya kura za urais Uhuru Kenyatta ana kura 5,219,456, huku mpinzani wake
wa karibu, Raila Odinga akiwa na 4,630,161 ya kura zilizohesabiwa.
Taarifa nyingine kutoka nchini humo
zilisema kuwa watu wameanza kurejea kazini licha ya bei za bidhaa kuanza
kuwa ghali kutokana na wafanyabiashara kupata hofu kwenda maeneo jirani
kununua vyakula hadi matokeo yatakapotangazwa.
Akizungumza katika Ukumbi wa Bomas jana,
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IECB), Ahmad Isaack
Hassan aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa kura
zinahesabiwa vizuri na matokeo yatatolewa baada ya kumalizika
kuhesabiwa.
‘’Najua mnachoka kusubiri, lakini zoezi
linaendelea vizuri na hakuna suala la wizi lililotokea mpaka sasa,
wananchi wa Kenya tuaminiane kwa hili,” alisema.
Aliongeza kuwa kura zanahesabiwa moja baada
ya nyingine chini ya ulinzi mkali, hivyo hakuna anayependelewa, wala
anayeonewa na haki inatendeka.
Aliwataka wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku kwa sababu zoezi karibia litakamilika muda siyo mrefu na pindi tu wakimaliza kuhesabu wanatangaza matokeo hayo.
Aliwataka wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku kwa sababu zoezi karibia litakamilika muda siyo mrefu na pindi tu wakimaliza kuhesabu wanatangaza matokeo hayo.
Katika hatua nyingine habari kutoka katika
kituo cha kuhesabia kura zinaeleza kuwa matokeo yatachelewa kutangazwa
kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika vituo vya kupigia kura 50.
MWANANCHI
MWANANCHI



No comments:
Post a Comment