Zaidi ya mashirika 12 ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake
kutoka mataifa ya kiarabu yameonya kuwa azimio la UN la kukabili
unyanyasaji wa wanawake linatishiwa na upinzani kutoka kwa chama cha
Muslim Brotherhood kutoka Misri, uongozi wa Vatican na Urusi.
Azimio hilo liko katika hatua za mwisho za mashauriano kabla ya
kuidhinishwa na tume ya kutetea maslahi ya wanawake katika Umoja huo.
Muslim Brtoher hood imesema kuwa azimio hilo
linatishia kuvuruga mpangilio katika jamii kwa kuwapa wanawake ruhusa ya
kusafiri, kufanya kazi au hata kupanga uzazi bila idhini ya waume wao.
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu
kutoka mataifa ya arabuni (hasa Misri, Lebanon Palestine, Jordan na
Tunisia) yametoa wito kwa mataifa yaliyo na uakilishi katika tume hiyo
ya UN juu ya haki za wanawake, yakome kutumia dini, utamaduni na mila
kama kisingizio cha kuruhusu ukiukaji wa haki na unyanyasaji wa
wanawake.
BBC SWAHILI



No comments:
Post a Comment