HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WANAKIJIJI WA MLOWE WAMZOMEA MKUU WA WILAYA YA MBOZI

 
Mkuu wa wilaya ya Mbozi  mkoani Mbeya  Dr. Michael Kadege  akiongea na wanakijiji cha Mlowo Mbozi
   
Baadhi ya wanakijiji wa Mlowo wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo
 
Wanausalama wakiwa makini kwa lolote litakalotokea 
 
 Mwanasheria wa halmashauri ya Mbozi akifafanua moja ya sheria za halmashauri hiyo 
  
Kauli hii ndio ilileta taflani “yeyote atakaezomea namtupa ndani” hapa ndipo hali ya hewa ilichafuka kwa wanakijiji wa Mlowo kumsikia mkuu wilaya akitamka hivyo.
  
Moja ya wanakijiji akimfuata mkuu huyo kumpokonya kiongeleo yaani kazi kubwa
 
Baadhi ya wanakijiji hicho cha Mlowo wakitulizwa na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho wapunguze jazba


Wanakijiji wakiondoka kwenye mkutano bila kufikia muhafaka wa jambo lao baada ya kutoelewana na Mkuu wa wilaya 
 
Mkuu wa wilaya akishauriana na moja ya wanakamati ya  ulinzi na usalama maana maelewano hakuna tena kwenye mkutano huo

Wakuu wakiondoka baada ya mkutano kuvunjika


 Kwa ujumla jeshi la polisi linabebeshwa mzigo ambao sio wake matatizo waanzishe wengine  kuja kutuliza wengine enyi mnaoanzisha matatizo jaribuni kuyamaliza wenyewe maana hapo mabomu yangepigwa lawama ingekuwa kwa jeshi la polisi  
Wanausalama wakiondoka katika mkutano uliovunjika ( Picha na Mbeya Yetu)


Mkuu wa wilaya ya Mbozi  mkoani Mbeya  Dr. Michael Kadege  amejikuta kwenye hali ngumu baada ya wananchi wa kijiji cha Mlowo kumzomea na kuvuruga mkutano wa kijiji ambao  ulikuwa na madhumuni ya kutatua mgogoro uliodumu kwa mwaka mmoja baina ya kijiji hicho na halmashauri ya wilaya kuhusiana na makusanyo ya ushuru kwa wafanya biashara.

Aidha wananchi hao wamepinga kitendo cha mkuu wa wilaya kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji bwana Daud Katule kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za kijiji , kutosoma mapato na matumizi pia kuchapisha vitabu vya kukusanya pesa na kutowasilisha fedha katika ofisi ya almashauri.

Kadege amesema sababu hizo ndizo zilimpelekea kumsimamisha uongozi bwana Katule na kwamba aliitwa kwenye kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi na halmashauri ya wilaya  ambapo imedaiwa kuwa alikiri kufuja pesa hizo na kuahidi atazirejesha lakini hakutekeleza hali iliypolekea kusimamishwa uongozi tangu Januari 2013.Kufuatia mvutano huo wananchi walifunga ofisi ya kijiji mwanzoni mwa wiki hii kushinikiza serikali kutatua mgogoro huo.

Mkuu wa wilaya ameagiza ofisi ifunguliwe mara moja ili shughuli za serikali ziendelee kama kawaida ambapo ofisi ilifunguliwa saa 10. 00 chini ya mtendaji kata Jackson Mwana na mtendaji kijiji Judhith mtega.

Hata hivyo mkutano huo ulidhibitiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambapo wananchi wamebaki hewani kwa kushindwa kutatuliwa mgogoro huo.

 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: