Pichani juu na chini ni baadhi ya
abiria wakiwa nje ya basi lao la Kilimanjaroo Express lenye namba za
usajili T860 BVA walilokuwa wamepanda wakitokea jijini Dar kuelekea
jijini Arusha mapema leo asubuhi,ajali hiyo imetokea eneo la Mombo
ambapo chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni dereva wa basi hilo
alikuwa akimkwepa muendesha baiskeli,matokeo yake basi hilo likakosa
mwelekeo na kupinduka,aidha katika jali hiyo inaelezwa kuwa watu kadhaa
wamejeruhiwa lakini hakuna aliyepoteza maisha.(Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog)





No comments:
Post a Comment