HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » YALIYOJIRI KWENYE KESI YA ASKARI ANAYETUHUMIWA KWA MAUWAJI YA MWANGOSI

 
 Mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi  akifichwa na askari kanzu  leo
 Hivi ndivyo askari  kanzu  walivyojaribu kumficha mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi leo
Huyu  ndie mtuhumiwa wa mauawaji ya Mwangosi (kulia) 
UPELELEZI  wa  kesi  mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa chanel ten mkoani
Iringa, marehemu Daud Mwangosi umeendelea  kupingwa  dana dana baada  ya  upande  wa jamhuri
kuomba  kesi hiyo ipangiwe  tarehe  nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi  wake 
kutokamilika . Katika  kesi hiyo ambayo mtuhumiwa  wake ni  askari  wa  kikosi  cha kutuliza ghasia mkoa  wa Iringa
(FFU) Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G 2573
Leo alifikishwa mahakamani hapo huku mkuu  wa  polisi wilaya (OCD) akiwazuia askari kuwazuia wanahabari kutimiza  wajibu  wao
Akisoma kesi hiyo mbele ya mwendesha mashitaka Adolf Maganga, hakimu
mkazi mwandamizi mfawidhi  wa  mkoa  Juma Hassan alisema kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo unahitajika muda zaidi kwa ajili ya uchunguzi wa kesi hiyo ya
mauaji.

Mtuhumiwa  Simon alifikishwa mahakamani hapo tofauti na ilivyokuwa  alipofikishwa kipindi kilichopita ambapo leo  alikuwa na askari kanzu wawili tu ambao  walikuwa  wakifanya jitihada za kumficha ili asipigwe  picha  Kesi hiyo itasomwa tena Machi 28,mwaka huu ambapo mtuhumiwa amerudishwa mahabusu.

Awali Februari 28, mwaka huu mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani na kusomewa kesi yake ”Chamber court”ambako waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia wala kusogea karibu eneo la chumba kilichokuwa kikisomewa kesi. Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo akiwa amezungukwa na askari kanzu wengi kama mahabusu wakilenga kukomesha waandishi wa habari wasipate picha mtuhumiwa huyo.
Akifikishwa mahakamani hapo, mtuhumiwa huyo alikuwa katika gari la mahabusu (karandinga) kama watuhumiwa wengine tofauti na siku za
mwanzo alipokuwa akifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari. 
Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa jambo lililoamsha hisia tofauti miongon

Katika hali isiyo ya kawaida, 14 Februari Mwaka huu mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 akiwa mahakamani hapo aliwatukana waandishi wa habari matusi ya nguoni kuwataka wasimpige picha huku akijidai kuwa muda si mrefu ataachiwa na kupambana na waandishi mitaani.

Siku hiyo(Februari 14,2012) Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema “mtapiga picha sana mtakavyo lakini hamjui kama kesho tu nitatoka halafu tupambane mitaani huko. Nawaona sana mnaonipiga picha tutakuja kukutana tu” alisema mtuhumiwa huyo.
 
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: