HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » YALIYOJIRI KWENYE MAZISHI YA HUGO CHAVEZ

Mwili wa Hugo Chavez ukiwa umewekwa kwenye jeneza kwa ajiri ya kuagwa kabla ya mazishi (1954 - 2013) 
Rais wa Argentina  Cristina Fernandez,kushoto ,  Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, wapili kushoto, Rais wa Uruguay  Jose Mujica,watatu kushotot, Rais wa Bolivia Evo Morales,wa nne kushoto,na mke wa Rais wa Uruguayan and Mujica's wife, Uruguaya  Senator Lucía Topolansky  wa kwanza kulia wakiwa mbele ya jenela lililobeba mwili wa rais Hugo Chavez
 
 Rais wa Cuba Raul Castro akimfariji mtoto wa Marehemu Rosa Virginia Chavez
 Rais wa Iran  Mahmoud Ahmadinejad akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Caracas
  Rais wa Cuba Raul Castro (katikati)  akitoa heshima kwa mwili  pembeni yake ni mtoto wa Rais Hugo Chaves  (Rosa Virginia Chavez) na Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro
Rais wa Brazil Dilma Rousseff,  na Rais wa zamani wa Brazil  Luiz Inacio Lula Da Silva wakitoa heshima zao kwa mwili wa Rais Hugo Chavesof Venezuela's late President Hugo Chavez.
 Mishumaa imewashwa katika  uwanja wa Simon Bolivar huko Sabaneta katika mji aliozaliwa Rais Hugo Chavez
 Rais wa Ecuador Rafael Correa, kushoto wakiwa na mkewe Anne Malherbe, wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Rais Hugo Chavez
 Kaka wa Rais Hugo Chavez Adan wa kwanza kushoto, Mama wa Rais Hugo Chavez Elena Frias wa tatu kushoto, Baba wa Rais Hugo Chavez Hugo wa pili kulia wakiwa mbele ya Jeneza
 ..................................
 Watu wa rika zote  wapata nafasi ya kutoa heshima  kwa mwili wa Rais Hugo Chavez


 

 



 
 Watu walipoteza fahamu baada ya kutizama mwili wa Hugo Chavez
Picha kwa hisani ya - EPA, AP, AFP/ Getty Image,Guardian.co.ukmiamiherald.comabc.net.
 .........................................
Serikali ya Venezuela imetangaza siku saba zaidi za maombolezi kabla ya kufanyika maziko ya marehemu rais wa nchi Hito Hugo Chavez baadaye leo.Serikali hiyo imeongeza muda wa maombolezi kufuatia kufurika zaidi watu wanaotaka kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

Makamu wa rais , Nicolas Maduro, amesema kuwa mwili wa bwana Chavez utakaushwa na baadae kuwekwa ndani ya kaburi la vioo ambapo utakuwa ukionekana.
Amesema kuwa serikali imeamua kuchelewesha uamuzi wa mazishi yake kwasababu zaidi ya raia milioni mbili wamekuwa wakipanga mstari kwa saa nyingi kwa ajili ya kupokea jeneza la chavez linalopita.

Maafisa wanasema kuwa bwana Maduro ataapiishwa kama rais wa mpito baadaye leo na uchaguzi kufanyika baadaye. Hugo Chavez, aliyeongoza Venezuela kwa miaka 14, alifariki baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili. Zaidi ya viongozi 30 kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Chavez baadaye leo akiwemo rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad, rais wa Cuba Raul Castro na rais wa Belarus Alexander Lukashenko.

Rais Ahmadinejad amemsifu Chavez kama mpigania haki na kiongozi mwenye kuleta mageuzi. Wabune wawili wa bunge la Congress la Marekani watawakilisha nchi hiyo katika mazishi haya ikikumbukwa kuwa Chavez alikuwa mkosoaji mkubwa wa Marekani.

BBC SWAHILI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: