AJALI MBAYA YA PIKI PIKI YATOKEA ASUBUHI HII BUGURUNI ROZANA, DAR
Ajali mbaya imetokea asubuhi hii ikihusisha pikipiki na daladala hii
ambazo zilikutana uso uso lakini Kwa BAHATI nzuri dereva wa pikipiki
Hiyo (mwenye helmet chini) alipona baada ya kuruka kwenye pikipiki na
pikipiki kuharibika vibaya baada ya kukanyagwa na gari. Picha kwa hisani
ya mwanaharakati mzalendo blog. Ajali za aina hii zimekuwa nyingi mno
jijini Dar es salaam na kwengineko kufuatia wimbi kubwa la bodaboda kila
mahali na uendesshaji usiofuata sheria
Balaa asubuhi
Askari wa trafiki wakiwa kazini baada ya ajali hiyo, huku dereva wa pikipiki akisubiri pembeni
Dereva wa pikipiki aliyenusurika
Polisi jamii na wasamaria wema wakijaribu kuinasua pikipiki uvungumi mwa daladala.Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog
Post a Comment