Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya
Magharibi Mkoa Mjini Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu }
akielezea mkasa uliompata wa kumwagiwa Tindi kali { Acid } mbele ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kumfariji.Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Sheha
wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Bwana Mohd Omar Said {
Maarufu Kidevu } anaendelea kupatiwa huduma za matibabu katika Hospitali
Kuu ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindi kali { Acid } na mtu
asiyejuilikana.
Mkasa
huo umempata jana usiku mara baada ya kurejea ibada ya sala ya Isha
wakati akiendelea na harakati za kutafuta huduma za maji na kumwagiwa
tindi kali hiyo iliyoathiri eneo la kifua chake, Bega pamoja na sehemu
za jicho la kulia.
Hili ni
tukio la tatu kutokea ndani ya mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha
aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma
pamoja na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman
Soraga.
Sheha
huyo wa Tomondo Bwana Mohd Omar Kidevu akizungumza na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Hospitali hapo kumfariji
pamoja na kumpa pole alisema alijikuta akimwagiwa tindi kali majira ya
saa 2.00 za usiku na mtu asiyemfahamu.
Bwana
Mohd Kidevu alisema Mtu huyo alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa
kufanya dhambi hiyo kitendo ambacho akalazimika kuomba msaada kwa
wasamaria wema lakini hatimae ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa
maumivu makali yenye kuchoma kama moto.
Sheha
huyo wa Shehia ya Tomondo aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba
hali yake hivi sasa inaendelea vyema na ameshaanza kupata matumaini
kufuatia jicho lake kuanza kuona ingawa bado anakabiliwa na maumivu
katika sehemu yake ya usoni.
Naye
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa
Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati wa kipindi hichi kigumu cha huduma
za matibabu.
Balozi
Seif alimuhakikishia Bwana Mohd Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itaendelea kufuatilia ushauri utakaotolewa na Madaktari kuhusu
tiba ya afya yake na kutoa msaada wowote utakaohitajika ili kuendeleza
nguvu za huduma ya tiba yake.
“
Tutafuatilia ushauri watakaotupa Madaktari kuhusu afya yao. Na kama kuna
wazo la kukusafirisha iwe Hospitali ya Rufaa Muhimbili au Nje ya Nchi
basi sisi kama Serikali tuko tayari kulitekeleza hilo “. Balozi Seif
alimuhakikishia Sheha Mohd Kidevu.
Akizungumza
na vyombo vya Habari nje ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe katika Hospitali
Kuu ya Mmnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Serikali Kuu imesikitishwa na vitendo hivi viovu
vinavyoleta athari kwa Binaadamu.
Balozi
Seif alisema tabia hii mbaya inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini
ikibeba ufinyu wa imani inaanza kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika
kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku.
Alisema
Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa
kufuatilia matukio hayo na haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa
kuwafikisha katika mkondo wa sheria.
No comments:
Post a Comment