Kocha wa Everton anayemaliza muda wake, David Moyes akienda kuaga kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Bill Kenwright leo alasiri.
Hapa Moyes akiingia ofisini kwa Kenwright kwa ajili ya mazungumzo ya kumuaga ili akasaini mkataba wa kuinoa Manchester United.
Moyes akitoka nje ya uzio wa ofisi ya Kenwright, baada ya kukamilisha mazungumzo ya kumuaga.
Huyoooooo akichanja mbuga kwa furaha baada ya kukubaliwa kuihama klabu hiyo akiwa amebakiza mktaba wa wiki sita .
Hapa kocha huyo 'anatroti' huku akionekana kama anayesema: Ngoja niwahi, wasije Man United wakachomoa kunipa ulaji bure!
Ni kama anasema: Siamini kama issue itakwenda kama navyotarajia.
MANCHESTER, England
Moyes, 50, ameingia mkataba
wa miaka sita kuifundisha Manchester United, kujaza nafasi inayoachwa na Sir
Alex Ferguson, aliyetwaa zaidi ya mataji 30 akiwa na Mashetani Wekundu hao,
yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya hapa
KLABU ya Manchester United, imeingia mkataba wa miaka sita
na kocha wa Everton anayemaliza muda wake David Moyes, ili kujaza pengo
linaloachwa na Sir Alex Ferguson.
Ferguson,
71, juzi alitangaza kustaafu kuinoa Man United mwishoni mwa amsimu akihitimisha
miaka 26 ya kufanya kazi na klabu hiyo Old Trafford.
Kutokana na uthibitisho wa Man United kumpa mkataba Moyes,
aliyebakiza wiki sita kwenye mkataba wake na Everton, kocha huyo anahitimisha
miaka 11 ya kuinoa klabu hiyo yenye makazi yake Goodison Park.
Moyes, 50, ameingia mkataba wa miaka sita kuifundisha
Manchester United, kujaza nafasi inayoachwa na Ferguson, aliyetwaa zaidi ya mataji 30 akiwa
na Mashetani Wekundu hao, yakiwamo 13 ya Ligi Kuu ya hapa.
"Sisi kwa kauli moja tumekubaliana na David
Moyes," alisema Ferguson.
"Moyes ni mtu mwadilifu, mwenye maadili imara ya kazi. Nimekuwa
mfuasi wa kazi zake kwa muda mrefu na nilimtaka aje hapa waka 1998 kujadili
naye juu ya nafasi ya kocha msaidizi.
"Hakuan maswali juu ya hili, ana sifa na viwango vyote
tunavyotarajia kutoka kwake kama kocha wa
klabu hii," Fergie alimuelezea Moyes.
Alasiri jana, Everton ilithibitisha katika taarifa yake
kuwa: "Everton inathibitisha kuwa Moyes ataondoka klabuni Goodison Park mwisho wa msimu.
"Alikutana na Mwenyekiti Bill Kenwright mapema alaasiri
ya leo na kuthibitisha kuwa anataka kujiunga Manchester United.
"Mwenyekiti kwa niaba ya klabu, anapenda kutoa shukrani
za dhati kwa Moyes kwa rekodi mbalimbali alizoweka tangu kutua kwake hapa Machi
2002," ilisomeka taarifa ya Everton.
Ferguson, ambaye atabaki
klabuni Old Trafford kama Mkurugenzi na Balozi,
amekuwa na uhusiano wa karibu mno na Moyes ambaye aliwahi kupendekeza awe
msaidizi wake wakati huo Moyes akiwa anainoa klabu ya Preston North End.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment