HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO WEMBLEY KUWAKARIBISHA BORUSSIA DORTMUND NA BAYERN MUNICH

Makao ya soka ya Uingereza yanaukaribisha mngurumo wa sauti za Wajerumani Jumamosi wakati Bayern Munich wakikwaruzana na Borussia Dortmund katika uga wa Wembley. Nani atalileta kombe Ujerumani?
Hiyo ni fainali ya kwanza kabisa kuwahi kuzileta pamoja timu mbili za Bundesliga katika historia ya Champions League. Ni miaka miwili tu iliyopita tangu Barcelona walipothibitisha hadhi yao katika soka la Ulaya kwa kuwabwaga Manchester United katika uwanja huo huo waliposhinda dimba hilo mwaka wa 2011, lakini namna ambavyo Bayern na Dortmund wamepenya katika kinyang'anyiro cha msimu huu inaashiria mpangilio mpya katika bara ulaya.
  Kikosi cha Borussia Dortmund kimeelekea London tayari kwa pambano la fainali uwanjani Wembley
 
Bayern iliwaacha Barecola wakiwa katika magofu baada ya kuwachabanga jumla ya magoli saba kwa sifuri katika nusu fainali, wakati ushindi wa Dortmund wa mabao manne kwa moja dhidi ya Real Madrid katika awamu hiyo uliwaacha ulimwengu wa soka vinywa wazi.
Bila kujali matokeo ya mechi ya leo, bila shaka utakuwa usiku wa kihistoria kwa soka la Ujerumani, lakini timu hizombili zinashuka dimbani zikiwa na motisha tofauti. Kwa Bayern, hiyo ni fursa ya kujikomboa kutokana na machungu waliyopata katika vichapo vya fainali za mwaka wa 2010 na hasa mwaka wa 2012 wakati walishindwa na Chelsea katika mikwaju ya penalti, fainali iliyochezwa kadamnasi ya mashabiki wao waliokosa kuamini macho yao katika uwanja wa nyumbani Allianz Arena.
Dortmund, waliofika fainali katika mwaka wa 1997, wanalenga kuwasababishia Bayern mashaka zaidi, ambao wamekuwa wakikandamiza kwa kiasi kikubwa juhudi za wapinzani wao kujiimarisha kuwa mahasimu wa muda mrefu, kwa kuwapokonya nyota wao mshambuliaji Mario Götze kwa kiasi kikubwa katika historia ya Bundesliga, euro milioni 37.
Fainali hiyo kati Bayern München na Borussia Dortmund inatarajiwa kujaa hisia kali ndani ya uwanja 
Fainali hiyo kati Bayern München na Borussia Dortmund inatarajiwa kujaa hisia kali ndani ya uwanja
 
Jeraha la mguu alilopata Götze limepunguza kitisho cha aibu ya kidiplomasia hii leo, lakini Bayern pia wanaamini kuendelea na harakati za kumpata mshambuliaji wa Dortmudn Mpoland Robert Lewandowski, ambaye aliiangamiza Madrid kwa kuwafinga magoli manne katika mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali.
Baada ya kushindwa mara tano mfululizo na Dortmund wakati wa ushindi wa taji la bundesliga misimu miwili mfululizo, mwaka wa 2011 na 2012, Bayern wametengeneza mambo msimu huu na kuepuka kichapo katika mechi zao zote nne za karibuni.
Mmoja wa mashabiki watakaofika katika uwanja wa Wembley ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ijapokuwa alipoulizwa ni timu ipi atakayoshabikia, hakuweza kuitaja yoyote ila akasema kuwa cha maana ni kwamba timu zote mbili zinatoka Ujerumani na vyovyote matokeo yatakavyokuwa, kombe la Chmapions League litapelekwa nyumbani.
 
UEFA yaiidhinisha hatua kali za kinidhamu
Katika habari nyingine za soka ya Ulaya ni kuwa Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya – UEFA Michel Platini, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua dhidi ya masuala matatu yanayotishia kabumbu: upangaji mechi, ubaguzi na vilabu kutumia fedha kupindukia. Akizungumza katika kongamano la UEFA jijini London jana, Platini amesema tatizo kubwa ni kupanga mechi na kuwekeana dau kwa sababu linawahusisha makundi makubwa yenye fedha.
 Rais wa UEFA Michel Platini anasema bado kuna mengi ya kufanywa ili kuutokomeza ubaguzi viwanjani 
Rais wa UEFA Michel Platini anasema bado kuna mengi ya kufanywa ili kuutokomeza ubaguzi viwanjani
 
Wachezaji watakaopatikana na hatia ya kuhusika na matukio ya kibaguzi katika mechi za vilabu barani Ulaya au za kimataifa watakabiliwa na adhabu ya chini ya kupigwa marufuku kucheza mechi kumi. Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Ulaya UEFA imeidhinisha hatua kali za kinidhamu.
Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino amesema vilabu vitakavyopatikana pia na hatia hiyo vitafungiwa viwanja vyao kwa sehemu Fulani kwa tukio la kwanza la ubaguzi wa rangi utakaofanywa na mashabiki wake, au viwanja vyao vifungwe kabisa kwa kosa la pili pamoja na faini ya euro 50,000. Imekubaliwa kuwa washindi wa taji la Europa LEAGUE watafuzu moja kwamoja kuanzia mwaka wa 2015 katika Champions League katika msimu utakaofuata. Uamuzi huo mpya unalenga kuimarisha na kuifanya Europa League kuwa yenye kuvutia kwa vilabu. Pia imekubaliwa kuwa timu 16 kutoka nchi 12 zitapewa vibali vya moja kwa moja vya kuanza katika awamu ya makundi ya kinyang'anyiro hicho. Kwa sasa timu sita kutoka mataifa sita hufuzu moja kwa moja katika awamu ya makundi ya Europa league.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef
DW IDHAA YA KISWAHILI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: