Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto
ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka
hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto
mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa
kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu
hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya
katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto
huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto
huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua
Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu
ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa
wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa
mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza
kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na
maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011
mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo
ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za
mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Aidha baada ya kuhojiwa alikiri
kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha
anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma
nyingine.
.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio
na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina
pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa
kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
Amesema mara baada ya watu hao
kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto
watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili
dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya
jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema
kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa
kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba
Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo
halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka
zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya
kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na
kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na
viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa
kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa
wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya
Inyala Kata ya Iyunga jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa
mtoto huyo wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na
kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo
kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa
kambo.
Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko
huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua
jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa
asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya
mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa
mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani
ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la
kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa
lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment