Vipi ndugu yangu, uenda wewe ni mzazi au unandugu yako mwenye umri wa
ujana, je ukimkuta anafanywa kama huyu hapa, utafanya nini, je utamtetea
au utamsaidiaje? ungetamani kuwambia nini wale wanaompa kipingo? je
utajitosha kumtetea? au utasema mpelekeni polisi?
wazazi tukae na watoto wetu kila wakati na kuwaonya wasitende maovu kama
vile wizi, huyu naye pia amezaliwa na anao wazazi, sijui wakiona yanayo
mpata mtoto wao inakuwaje moyoni mwao, uchungu!!
Tunaambiwa kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa, je ndugu yetu kama
huyu baada ya kifo hiki kinachotokana wizi anakwenda wapi! je
amefanikiwa kuomba msamaha katika mateso haya?
Jamani ni vema kukumbuka kwamba hatupaswi kuua katika maisha yetu, Mungu
anasema Usiue, hata kama tumefanyiwa jambo baya, hata kama mwizi
katuibia, tusiue, mpeni nafasi ya kutubu, kuua ni jambo baya sana
kwasababu ukimwaga damu ya mtu kwa kuua ile damu uliyoimwaga uwa
inazungumza mengi na kulia sana juu ya yule anayefanya kitendo kile,
inaweza kulipa kisasi na pengine kutamka laana!!
PICHA NA SAUTI YA KANISA
No comments:
Post a Comment