Dar es Salaam. Wanasayansi nchini Marekani
wamebaini kifaa kipya kitakachoharakisha upatikanaji wa chanjo ya virusi
vya Ukimwi (VVU).
Taarifa kwa Mwananchi Jumapili iliyotolewa
Alhamisi wiki hii na Taasisi ya Tafiti Kukabiliana na Magonjwa ya Mzio
na Kuambukiza (NIAID) ya nchini Marekani ilieleza kuwa mfumo wa kifaa
hicho siyo tu utasaidia kurahisisha chanjo kukabiliana na VVU, bali hata
kwa magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi kama mafua na yale
yanayosababisha uvimbe wa ini.
“Ni mfumo wa hali ya juu wenye uwezo wa haraka wa
kuchambua chembechembe kinga zenye uwezo wa kuangamiza aina mbalimbali
za VVU zinazopatikana duniani,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliyoambatanisha majina ya
wanasayansi nguli wa NIAID ambao wamethibitisha kifaa hicho chenye mfumo
mpya katika teknolojia ya kuchambua VVU, umeweka wazi kuwa matatizo
waliyokuwa wakipata wanasayansi katika kudhibiti virusi sasa imepata
ufumbuzi.
Uzuri wa kifaa hicho unaelezwa kwamba ni kuweza
kuchambua na kutofautisha chembe kinga za aina mbalimbali, hata kujua
idadi na uwezo wake katika kushambulia adui katika mwili wa binadamu.
“Uchambuzi wa kifaa hiki unaweza kutumika
kuchunguza namna mwili wa binadamu unavyoweza kukabili maradhi mengine
yanayosababishwa na virusi kama vile mafua na uvimbe wa ini,” anaeleza
sehemu ya taarifa hiyo.
Wanasayansi nguli wa NIAID waliothibitisha uwezo
wa kifaa hicho ni Mtaalamu wa Dawa na Mifumo ya Kibiolojia, ambaye pia
ni Mkuu wa Idara ya Chanjo, Profesa Peter Kwong na Mkuu wa Idara ya
Kinga, Profesa John Mascola.
Wataalamu hao wanaeleza kuwa kifaa hicho kina
uwezo wa kutofautisha ni chembechembe gani za kinga zenye uwezo wa juu
katika kukabili virusi vya maradhi.
Kupitia njia hiyo, inaelezwa kuwa ni rahisi
kubaini chanjo yenye nguvu, hivyo kuharakisha upatikanaji wa chanjo
itakayothibitishwa kukabiliana na VVU.
Kulingana na teknolojia na tafiti mbalimbali, VVU
bado hajaipata tiba au chanjo madhubuti, ingawa wameweza kupata dawa
zenye uwezo mkubwa wa kupunguza makali ya virusi hivyo (ARVs).
Hadi sasa tafiti mbalimbali zimeonyesha uwezekano wa kupatikana tiba na chanjo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kwa sasa tafiti nyingi zipo kwenye majaribio,
NIAID inaeleza kuwa kupatikana kwa kifaa hicho kutaharakisha kazi ya
kuchanganua uwezo wa chanjo hizo katika kukabiliana na VVU.
Kauli ya Serikali
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid ameelezea kuwa ugunduzi huo ni ukombozi kwa dunia katika kuharakisha upatikanaji wa chanjo ya VVU.
Taasisi hiyo ya utafiti inaeleza kuwa mfumo wa kifaa
kilichokuwepo awali, haukuwa na uwezo wa kuchambua kiufasaha chembe
kinga mbalimbali wala umahiri katika kukabiliana na virusi.
“Hata hivyo, kwa sasa itakuwa rahisi kuchambua
sampuli za damu, hata kutofautisha makabiliano dhidi ya virusi kulingana
na makusudio yetu.
Awali hatukuwa na teknolojia ya kufanya hivyo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya NIAID.
Kwa jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi,
walikifananisha na mashine ya kutambua alama za vidole kinachoweza
kutofautisha watu bila kukosea.
Kulingana na taarifa ya watafiti hao, kifaa hicho
kina uwezo wa haraka wa kufanya kazi hata kwa kutumia kiwango kidogo cha
damu, kuliko njia nyingine zozote.
Ugonjwa wa Ukimwi iligundulika miaka 30 iliyopita,
hadi sasa umeua watu wengi na kusababisha kupungua kwa nguvukazi pamoja
na wataalamu wa sekta mbalimbali hasa katika nchi maskini.
Kauli ya Serikali
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid ameelezea kuwa ugunduzi huo ni ukombozi kwa dunia katika kuharakisha upatikanaji wa chanjo ya VVU.
“Ni jambo zuri hasa katika kuharakisha upatikanaji
huo wa chanjo… Maana virusi (VVU) hawa wamekuwa na tabia ya
kubadilikabadilika, hata kufanya iwe kazi ngumu kupata antibodies
(chembe kinga) watakaosaidia mwili kupambana na virusi wa Ukimwi,”
alisema Dk Rashid.
Alikiri kuwa zipo tafiti mbalimbali za chanjo ya
Ukimwi duniani, lakini zimekuwa zikisuasua kutokana na ugumu wa vifaa
madhubuti vya kuchunguza mwenendo wa chembe kinga, hata uwezo wake,
hivyo kazi hiyo kuchukua muda mrefu.
Dk Rashid akasema, ugunduzi kama huo ni muhimu kwa wakati huu ambapo kuna juhudi za kutafuta tiba na chanjo ya Ukimwi.
Kuhusu juhudi za Serikali kupata kifaa hicho ili
kuharakisha shughuli za utafiti nchini, Dk Rashid alisema kuwa taratibu
zake ni hadi pale kitakapothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alisema vifaa vyovyote vinavyohusiana na tiba
vinaweza kuingizwa nchini baada ya kupata maelezo na umuhimu wake katika
kulisaidia taifa kwa uthibitisho wa WHO.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
(Tacaids) Dk Raphael Kalinga alisema iwapo wanasayasni hao watakuwa
wamefanikiwa katika hilo ni mafanikio katika teknolojia ya kukabiliana
na VVU.
“Ni hatua nzuri,” alisema Dk Kalinga akisisitiza kuwa ni jambo linaloinufaisha dunia na hakuna anayeweza kukataa maendeleo.
Pamoja na pongezi hizo, Dk Kalinga alisema
ugunduzi wa aina hiyo utasaidia zaidi, hasa uchunguzi kwa watoto
wachanga, ambao kazi yake imekuwa ngumu ukilinganisha na watu wazima.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment