Mahakama
Kuu ya Tanzania imefuta mashitaka yote ya ugaidi yaliyokuwa
yanawakabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare
na mwenziye Ludovick Joseph.Taarifa
zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la kula njama ya
kuteka na kudhuru, kosa ambalo kimsingi ni la jinai na lenye dhamana.
Taarifa zaidi zinasema kuwa watuhumiwa wamerudishwa rumande kwa kuwa dhamana haikuwa imeandaliwa.
Katika kesi hii, Lwakatare anawakilishwa na jopo la mawakili watano ambao ni Mabere Marando, Tundu Lissu, Prof. Abdallah Safari, Peter Kibatala na Nyaronyo Kicheere.

No comments:
Post a Comment